TAARIFA KUHUSU MAHOJIANO LOWASSA ALIYOFANYA KITUO CHA POLISI LEO

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa ameruhusiwa kutoka katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam baada ya kuhojiwa na kisha kujidhamini.
Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amehojiwa kuhusu tuhuma za uchochezi zinazomkabili na akaruhusiwa kuondoka ambapo ametakiwa kurejea tena siku ya Alhamisi.
Kwa mujibu wa Wakili Peter Kibatala, sababu za kuhojiwa kwa Lowassa ni juu ya kauli alizozitoa wakati wa futari alipokuwa akiongea na waumini wa dini ya kiislam.
Miongoni mwa mambo mengi aliyozungumza Lowassa katika futari hiyo ni kuhusu Masheikh wa Uamisho wanaoshikiliwa na serikali kwa miaka minne sasa dhidi ya tuhuma za ugaidi.
Lowassa alipewa wito huo jana, ambapo tangu alipofika katika kituo hicho cha polisi leo asubuhi, ulinzi umeimarishwa kufuatia wingi wa waandishi wa habari na watu wengine waliokuwa wamekusanyika jirani na kituo hicho.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sZtUsw
via IFTTT