Ramadhan Singano aigomea Azam Fc.

KIUNGO wa Azam FC, Ramadhan Singano ‘Messi’ amegoma kuongeza mkataba kwenye timu yake baada ya kupunguziwa mshahara.
Singano alijiunga na Azam Julai 8, mwaka juzi akitokea kwenye klabu ya Simba kwa ada ya milioni 40 huku akiwa analipwa mshahara wa milioni 2 kwa mwezi.
Mkataba wa mchezaji huyo unaisha Julai 8, mwaka huu hivyo katika harakati za kumuongezea mkataba mpya kumetokea lugha gongana Azam na Singano jambo linaloweza kumfanya mchezaji huyo kutimka ndani ya klabu hiyo muda wowote.
Kutokana na ukata wa fedha unaoikabili timu hiyo, Azam FC wamempa ofa ya kusaini mkataba wa miaka miwili Kwa dau la milioni 10 na mshahara wa 1,150,000 Kwa mwezi. 
Singano amegomea kupunguziwa mshahara wake ndani ya klabu hiyo hivyo hadi sasa hakuna maelewano mazuri baina ya mchezaji huyo na timu yake. Shaffiidauda.co.tz. imebaini.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2soWPHr
via IFTTT