MASWALI YA KUJIULIZA KABLA YA KUANZA UHUSIANO WA KIMAPENZI

Kabla hujaoa au kuolewa, kuna mambo unayotakiwa kuongea na mwenza wako. Mnaweza kuamua kwenda ufukweni au mahali tulivu na muongee kuhusu maisha yenu yatakavyokuwa. Hii yaweza isiwe njia iliyozoeleka ya kujiandaa na ndoa lakini kwako na mwenza wanko, ikafanya kazi.
Sikutaka tu kuongelea mambo kama mtapataje pesa au wapi mtaishi, bali mkae na kujiuliza endapo kweli mpo tayari kuanza maisha ya pamoja.
Labda wewe haupo kwenye hatua hiyo kwa sasa, lakini unafikiria kuingia kwenye uhusiano wa kudumu wa kimapenzi baada ya kuwa peke yako kwa muda mrefu. Kabla hujajiingiza huko, kuna maswali machache yabidi ujiulize kwanza:
1. Je, nina furaha hata kabla sijaingia kwenye uhusiano?
Yawezekana ikakuchanganya, lakini ili uwe na maisha ya furaha na mtu mwengine, ni lazima uwe ni mtu mwenye furaha hata unapokuwa mwenyewe. Isiwe kwamba furaha hiyo unayoitaka itoke kwa mtu mwingine.
Ni vizuri kuwa na mwenza wa kuwa nae pamoja kimaisha lakini kuanza uhusiano mpya wa kimapenzi haitasaidia kutatua matatizo yako binafsi uliyonayo kwa sasa. Hii haijalishi kama matatizo hayo ni ya nje tu kama kutokuwa na pesa au yawe ni matatizo yako ya ndani kama hisia zako za upweke ambazo unazo toka utotoni mwako, kuongeza mtu mwingine maishani mwako kutafanya matatizo yako yawe makubwa zaidi, sio kuyaondoa.
Kabla hujajiingiaza kwenye uhusiano wa kudumu wa kimapenzi, hakikisha kwamba mambo yapo sawa kwenye maisha yako – kusiwe na mambo yanayomsumbua hisia zako. Ukishajua kwamba una furaha hasa, afya nzuri, na unajisikia vizuri, hapo utakuwa kwenye nafasi nzuri kumfanya mtu mwingine aingie maishani mwako.
2. Je, kuna kitu nitakachokipata baada kwa kuingia kwenye ndoa ambacho kwa sasa sina?
Maisha yako hayana muelekeo kwa sasa? Kazi imeanza kukuchosha? Mtu uliyekuwa unaishi naye ameondoka na sasa umebaki peke yako, kwa hiyo sasa ni bora utafute mpenzi ili usiwe mpweke?
Kama kuna jambo hata moja linakuelezea wewe zaidi, basi ujue suluhisho la matatizo yako yawezekana isiwe kutafuta mpenzi. Yawezekana tu kwamba kuna mambo yamekuchosha maishani.
Kuingia kwenye uhusiano wa kudumu kisa kuna kitu hakiendi sawa maishani mwako, kama furaha ya maisha, basi kujiingiza kwenye mahusiano ya kudumu kimapenzi sio suluhisho la matatizo yako. Baada ya muda mfupi utajikuta unamshinikiza mpenzi wako mara kwa mara atumie muda mwingi kukufanya wewe uwe mchangamfu, au utaishia kuboreka kwa sababu toka mwanzo ulichohitaji sio mapenzi ya kudumu bali mtu wa kukuchangamsha tu.
Usijiingize kwenye mapenzi kwakuwa huna mambo ya kufanya. Kuna klabu nyingi tu kwa ajili ya kutatua hilo.
3. Nina muda wa kutosha?
Ni muhimu ujiulize iwapo una muda wa kutosha kwa ajili ya uhusiano – sio kwa sasa tu, ila pia kama utakuwa na muda endapo uhusiano wenu utadumu na kukua. Yawezekana kwa sasa ukawa na muda wa kutosha, lakini utakuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya mpenzi wako wakati uhusiano wenu utapokuwa imara zaidi?
Kama unahitaji uhusiano wa kimapenzi na mtu fulani kwa sababu sahihi, bila shaka muda utapatikana tu, hata kama umebanwa na shughuli nyingi kiasi gani. Kwahiyo ni wewe wa kuhakikisha kuwa unaweza kutenga muda huo kwa ajili ya mpenzi wako, la sivyo shughuli zako za siku nzima tu zinahitaji muda zaidi ya uliopo ndani ya siku kuzitimiza.
4. Je, nipo tayari kubadilika?
Uhusiano ni mzuri sana, lakini pia una kazi kubwa ndani yake.
Kama kiwango chako cha uvumilivu ni cha chini, kujiingiza kwenye jambo litalokuhitaji uache mambo mengi uliyoyazoea na uwe tayari kubadilika yaweza usiwe uamuzi bora kwako. Kuingia kwenye uhusiano wa kudumu kutabadili masiha yako moja kwa moja. Kimsingi, inapotokea jambo lolote jipya likaingia maishani mwako, tegemea kwamba litakuhitaji ubadilike.
Uhusiano mara nyingi unakulazimisha kuwa wazi kupokea mabadiliko ya mara kwa mara. Sio tu mabadiliko ya mambo makubwa kama mahali utapokwenda kuishi au muda gani utakuwa na familia yako. Pia yatahusu mambo madogo kama kukubali kwenda kwenye hoteli fulani kula chakula anachopenda mwenza wako huku wewe ukiwa unatamani kuwa hoteli tofauti na hiyo ukila chakula kingine.
Kabla hujaingia kwenye uhusiano wa kudumu, lazima ujiulize iwapo upo tayari kubadilika kwa ajili ya mwenza wako itapokubidi kufanya hivyo.
5. Je, ni kweli nahitaji mahusiano ya kudumu?
Ni lazima ujiulize hasa sababu ya wewe kutaka mahusiano ya kudumu ya mapenzi.
Wengi wetu hata hatuna hakika ni kitu gani hasa tunataka maishani, lakini tunajikuta kwenye mahusiano ya kudumu hata kabla hatujajua tumeingiaje. Ingia kwenye uhusiano kwa kudumu kwakuwa unataka kufanya hivyo, umeamua kutulia na kwamba upo tayari kuanza maisha ya pamoja na mtu mwingine – raha na shida.
Kauli “uhusiano wa kudumu” yaweza kuwa na maana tofauti kwa watu tofauti. “Wa kudumu” yaweza kumaanisha ndoa na watoto kwa mtu mmoja, na kwa mwingine ikamaanisha kupata mtu ambaye ataweza kutoka naye muda wowote. Ni muhimu kujua unachotarajiwa kutoka kwenye uhusiano unaoutaka.”
Kwa maana nyingine, unatakiwa ujue wazi unachofanya na sababu ya kukifanya.
Kuwa kwenye uhusiano wa kudumu ni jambo zuri sana, lakini inabidi uwe tayari kwa asilimia 100. Kama huna hakika ni bora ujiulize maswali hayo kwanza na utathmini uamuzi unaotaka kuufanya.

from Blogger http://ift.tt/2tFrlf6
via IFTTT