Marekani Yaishambulia na Kuiangusha Ndege isiyo na Rubani Nchini Syria

Ndege ya jeshi la Marekani imeangusha ndege isiyo na rubani inayoendeshwa na serikali ya Syria kusini mwa nchi, Ndege hiyo isiyo na rubani ilidaiwa kuwa na silaha na ilikuwa hatari kwa jeshi la Marekani ardhini.
Hiki ni kisa cha karibuni kabisa katika anga ya Syria, baada ya Marekani kuangusha ndege ya kivita ya Syria siku ya Jumapili na ndege nyingine isiyo na rubani mapema mwezi huu.
Katika taarifa nyingine jeshi la Marekani lilitangaza rasmi kuwa lilimuua kiongozi wa cheo cha ju wa kundi la Islamic State Turki al-Binali, wakati wa shambulizi lililofanywa na ndege nchini Syria Mwezi uliopita.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rBFPLy
via IFTTT