Lewis Hamilton ampoteza kabisa Sebastian Vettel kwenye Canadian Grand Prix.

Mercedes-AMG’s British driver Lewis Hamilton celebrates on the podium at the Yas Marina circuit in Abu Dhabi on November 23, 2014 after the Abu Dhabi Formula One Grand Prix. AFP PHOTO / KARIM SAHIB (Photo credit should read KARIM SAHIB/AFP/Getty Images)
Upinzani kati ya madereva wawili mmoja kutoka Mercedes na mwingine kutoka Ferrari lilikuwa ni kati ya mambo yaliyovuta hisia na macho ya watazamaji wengi katika mbio za rangaranga zilizofanyika usiku wa jana za Canadian Grand Prix huku wengi wakitaka kuona nani ataibuka mbabe.
Lakini Muingereza Lewis Hamiliton kutoka Mercedes alimkalisha Sebastian Vettel wa Ferrari ambaye anatajwa kama mpizani wake mkubwa baada ya Hamilton kuibuka kidedea katika michuano hiyo huku akimuacha mbali Sebastian Vettel ambaye aliishia kushika nafasi ya nne katika mbio hizo.
Huu ulikuwa ushindi wa sita kwa Hamilton katika Circuit Gilles Villeneuve lakini nyuma ya Hamilton aliyemaliza nafasi ya pili alikuwa dereva mwenzake kutoka Mercedes Valtteri Bottas huku aliyeshika nafasi ya tatu akiwa ni dereva kutoka katika timu ya Redbull Daniel Ricciardo.
Hamilton ambaye mwaka 2007 alishawahi kushinda tena katika barabara hiyo kwa mara ya kwanza alisema “hakika nahitaji kila mwisho wa wiki uwe kama hivi kwani tukio hili linanikumbusha mwaka 2007 nimefurahi kuendesha gari hii na hakika nimefurahia mashindano haya”
Lakini pamoja na Hamilton kushinda mashindano hayo ila Sebastian Vettel bado anaongoza msimamo wa madereva wa Formula One huku Lewis Hamilton akiwa katika nafasi ya pili, Valteri Bottas anashika nadasi ya tatu huku nafasi ya nne ikishikiliwa na Kim Raikkonen kutoka timu ya Ferrari.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2st06qb
via IFTTT