Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa jana alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano.
Lowassa ambaye pia amewahi kuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, hakupewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.
Licha ya kutoelezwa dhumuni la wito wote, kumekuwapo na tetesi ambazo hata yeye amekiri kuwa, huenda wito huo umetokana na kauli aliyoitoa mwishoni mwa juma kuhusu Masheikh wa Uamisho ambao wanashikiliwa na serikali kwa miaka minne sasa.
Akiwa katika futari hiyo aliyoalikwa, Lowassa alisema kuwa alipokuwa akigombea urais mwaka 2015, aliahidi kwamba, kama angeshinda, siku hiyo hiyo angewaachia viongozi hao wadini wanaoshikiliwa. Lakini kwa vile hakushinda, alimsihi Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo la viongozi wanaoshikiliwa kwa miaka yote hiyo bila kesi.
Mbali na hilo, Lowassa aliwataka waislamu kutokuwa wa baridi sana, badala yake watafute lugha nyingine ya kuzungumza ambayo serikali itasikia ili kuachia viongozi wao wanaoshikiliwa. Jambo hili huenda ndilo lililopelekea Lowassa kuitwa, kwani lina sura ya uchochezi ndani yake.
Lowassa awataka Waislam watumie lugha nyingine ili serikali iwaachie Masheikh wa Uamsho wanaoshikiliwa kwa miaka minne sasa. http://pic.twitter.com/430BS2dvXK— Swahili Times (@swahilitimes) June 26, 2017
Masheikh wa Uamisho wanaoshikiliwa nchini walikamatwa Zanzibar ambapo wanatuhumiwa kwa ugaidi.
from Blogger http://ift.tt/2sLSWN2
via IFTTT