Haya ndio maamuzi kisheria ya Kagera Sugar dhidi ya Mbaraka na Azam FC

Siku mbili baada ya Azam kutangaza kumsajili mshambuliaji Mbaraka Yusuph, uongozi wa Klabu ya Kagera Sugar alikotokea mchezaji huyo umeibuka na kupinga usajili huo, huku ukipanga kupeleka madai yake TFF.Kagera Sugar inapinga usajili huo kwa madai kuwa bado mchezaji huyo ana mkataba na wakata miwa hao wa Kagera.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, uongozi wa klabu hiyo ukiongozwa na meneja wake, Mohamed Hussein hivi sasa unaelekea katika Shirikisho la Soka Tanzania TFF kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko rasmi.
Mbaraka ambaye amefunga mabao 12 katika msimu uliomalizika wa ligi, amekuwa akiwaniwa pia na Yanga, huku Kagera wakitaka kumbakiza mikononi mwao, lakini Azam wamefanikiwa kunasa saini yake kwa mkataba wa miaka miwili.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2riCo0c
via IFTTT