Florentino Perez afunguka kuhusu Ronaldo,Mbappe,Morata na Zidane.

Real Madrid imekuwa ikiandikwa sana katika kurasa za mbele za magazeti na vyombo mbalimbali vya habari huku kubwa likiwa ni mwanasoka bora wao Cristiano Ronaldo kutishia kuondoka katika klabu hiyo.
Raisi wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez kwa mara ya kwanza amefungua kinywa chake na kuelezea kuhusu tishio la Ronaldo kuihama klabu hiyo na pia kuhusu kumsajili Kylian Mbappe kutoka klabu ya Monaco.
Perez ameshimdwa kuwahakikishia mashabiki wa Real Madrid kam a Ronaldo anaweza kubaki katika klabu hiyo au ataondoka na kuishia tu kusema kwamba “ninachokijua mimi ni kwamba Cristiano Ronaldo ni mchezaji wetu”
Lakini Perez amekiri kwamba raisi wa PSG ni rafiki yake mkubwa lakini hajawahi kuongea naye kuhusu Ronaldo, kauli hiyo inawafanya Manchester United kubaki kama klabu pekee inayomtaka Ronaldo.
Perez amesema sio vyema kumzungumzia Ronaldo kwa sasa wakati yuko na majukumu makubwa ya timu ya taifa na hataki kuwakwaza timu ya taifa ya Ureno kwahiyo kuhusu uhamisho wa Ronaldo atauzungumzia baada ya mashindano hayo kuisha.
Kuhusu Kylian Mbape raisi huyo wa Real Madrid amekiri kwamba Mbappe ni mchezaji mzuri sana na wao kama Real Madrid wamekuwa wakimfuatilia ili kuona ni nini wanaweza kufanya kuhusu yeye japo amekiri bado sana kwa wao kumnunja Mbappe.
Kuhusu Alvaro Morata raisi huyo amesema kwamba wao hawataki Morata aondoke na mchezaji mwenyewe pia hakuwahi kusema kwamba anataka kuondoka na habari zinazoandikwa mtandaoni sio kweli.
Lakini la mwisho ambalo Florentino Perez amelizungumzia ni kuhusu tetesi za Zidane kuondoka ambapo amesema wao hawajui kuhusu kuondoka kwake na wanajipanga kumsainisha mkataba mpya.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sOXe6X
via IFTTT