Beki wa Klabu ya Liverpool Mamadou Sakho Atua Tanzania Kimyakimya na Kujichimbia Arusha..!!!

Beki wa Liverpool anayetakiwa na Crystal Palace, Mamadou Sakho ametua Arusha akiwa njia kutembelea mbuga za wanyama.
Sakho anafuata nyayo za David Beckham aliyekuwa nchini wiki iliyopita na kutembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti.
Sakho alipoteza mvuto katika kikosi cha Liverpool chini ya kocha Jurgen Klopp aliyeamua kumtoa kwa mkopo Crystal Palace mapema Februari.
Hata hivyo, dau la pauni 30 milioni wanalotaka Liverpool linaonekana kumshinda mwenyekiti wa Palace, Steve Parish akisema fedha hizo nyingi kwao.

from Blogger http://ift.tt/2rWysBV
via IFTTT