Uwezo wa Kujibu Maswali ya Interview Unaombeba Diamond Platnumz

HE IS THE MASTER OF ANSWERS NA KAMA KUNA KITU AMBACHO KINAFANYA INTERVIEW NYINGI ZA Diam ZIWE NA MVUTO NI UWEZO MKUBWA ALIONAO WA KUJIBU MASWALI HASA LINAPOKUJA SWALA LA KUULIZWA KUHUSU UTOFAUTI BAINA YAKE NA MTU FLANI.
Naweza kiri kabisa kuwa Diamond amekuwa anajitahidi sana ku hannd dle maswali yanayohusu yeye na Ali Kiba na anapojibu amekuwa anaweka kwanza u Tanzania mbele na kuhakikisha anazuia watu kutumia matatizo yao kama njia ya wao kufanikisha mambo yao.
Nakumbuka kwenye XXL kipindi kile ndio ametoka kutupiwa makopo kwenye fiesta alifanyiwa interview na akaulizwa juu ya kile kilichotokea watu wakiwa wanafikiri diamond atasema wale waliorusha makopo ni watu wametumwa na hasimu wake alijibu tofauti kabisa kitu kilichofanya kila mtu ashangae jinsi alivyokuwa mtulivu wakati wa kujibu mpaka nakumbuka Adam Mchomvu alikiri kuwa majibu ya Diamond ni majibu ambayo huwezi yategemea kuwa yanajibiwa na mtu ambaye ametoka kuzomewa.
Diamond naamini kungekuwa na tuzo ya kujibu maswali angekuwa ashapewa nyingi.Ila kitu cha msingi kwake anaendeshwa na busara na hekima sio hisia mana ukiwa ubafanya interview halafu unajibu kwa hisia zako eidha za chuki ndio mwisho wa siku mtu anapaniki.
KATIKA REKODI YANGU SIJAWAHI KUONA DIAMOND AMEPANIKI KWENYE INTERVIEW HATA SWALI LIWE LAKUKERA KIASI GANI.
MASWALI ANAYOKUTANA NAYO DIAMOND KUHUSU MUZIKI,MAISHA YAKE YA MAHUSIANO,FAMILIA KWA UJUMLA NA KASHFA ANAZOZUSHIWA ANGEKUWA HAJAPEWA UTULIVU NA HEKIMA KUNA KILA SIKU ANGEKUWA ANAGOMBANA NA WATANGAZAJI NA KUSUSIA MAHOJIANO. 
By Abby

from Blogger http://ift.tt/2rc0cPX
via IFTTT