Steve Nyerere, Faiza Wazungumzia Kifo Cha Ivan Don

Waigizaji kutoka Bongo Movie, Steve Nyerere na Faiza Ally kwa nyakati tofauti wamezungumzia kifo cha aliyekuwa mume wa zamani wa Zari ‘Ivan’ aliyefariki hapo jana.
Waigizaji hao kila mmoja amedai amejifunza kitu kutoka katika maisha ya Ivan.
Steve Nyerere ameandika,
“Alikuwa na pesa nyingi, alikuwa na uwezo wa kufanya chochote, alikuwa na uwezo wa kununua chochote lakini ameshindwa kununua uhai. Nimejifunza kitu kupitia wewe, tuishi vizuri na watu maana hakuna ajuaye kesho,”.
Kwa upande wake Faiza Ally ameandika ujumbe mrefu usemao,
“Binaadamu akikuchukia hata zuri kwake ni baya na ndio maana huwa na maisha yangu tu kama mimi bila kutaka kuwa yoyote, hakuna zuri mbele ya mtu mbaya. Unajua nini wala sijali naona upuuzi tu kama ya kipuuzi mengine yote yalio pita..Maisha yangu na wanangu yako kwenye mikono salama hata kushinda mikono yangu, yako kwenye mikono ya Mungu mwingi wa rehma. Leo Ivan na matajiri wengine wako wapi? Mali sio kila kitu kwenye maisha yetu tunahitaji amani, mapenzi, maelewano makubaliano.
Nimetoka kwenye kutokua na mlo mpaka sasa namiliki milo, huo ni utajiri mkubwa maana kwanza ni kushiba akili ikae sawa ndio upange habari zingine, so at the end my heart is pure and that what give me amani ya moyo, hayo mengineyo tena yako nje ya uwezo wangu ni mipango ya Mungu”

from Blogger http://ift.tt/2r77nsM
via IFTTT