Rais Paul Kagame wa Rwanda, ametangaza azma yake ya kun’gatuka madarakani baada ya mwaka 2024.
Rais Kagame amethibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa Jeune Afrique kuwa awamu hii ya miaka saba ndiyo ya mwisho na Wanyarwanda wanatakiwa waanze kufikiria mtu mwingine atakayewaongoza baada ya mwaka 2024.
Rais Kagame ameuambia mtandao wa Jean Afrique, kwamba, muda muafaka wa kupumzika umewadia na amewaomba raia wa nchi hiyo waanze kufikiri nje ya mimi baada ya miaka saba.
Kwa sasa hakuna shaka yoyote kuwa Rais Kagame atashinda uchaguzi wa urais wa Agosti 3 mwaka huu na ni ushindi ambao umekuwa ukitabiriwa kwa muda mrefu na Wanyarwanda.
Mwaka 2015 Wanyarwanda wapatao milioni 4 ambao ni zaidi ya asilimia 70% ya wapiga kura, walipaza sauti zao kulitaka Bunge lirekebishe Katiba ili RaisKagame apate nafasi ya kuendelea kutawala.
Bunge lilifanya hivyo ili kumruhusu Rais huyo ambaye ana umri wa miaka 59 kuwania muhula mwingine..
from Blogger http://ift.tt/2s6Ua2d
via IFTTT