Picha zote za ajali ya Jonas Mkude wa Simba

NAHODHA wa Mabingwa wa kombe la Shirikisho na Kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo ilipotokea ajali hiyo, Dumila katika shamba la Mitiki, zinaarifu kuwa kuna watu wawili ambao bado majina yao hajapatikana wameumia na Mkude kupata majeraha madogo na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Watu hao walikuwa katika gari aina ya Toyota VX lenye namba za Usajili T 834BLZ na walikuwa wakitokea Dodoma kushuhudia fainali za kombe la Shirikisho la Soka Tanzania uliopigwa jana katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma uliozikutanisha Simba na Mbao.
Simba ilishinda mchezo huo kwa bao 2-1 na kutwaa ubingwa huo na kujipatoia tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Chanzo: Daily News Blog

from Blogger http://ift.tt/2qubCxj
via IFTTT