Wayne Rooney ameachwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kwa sababu, kuna wachezaji wengine wana viwango zaidi yake, anasema kocha wa Uingereza Gareth Southgate.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United hajajumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 kilichotangazwa leo kwa ajili ya michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu za Scotland na Ufaransa mwezi ujao.
Rooney pia aliachwa kwenye cha Uingereza, mwezi Machi kwa sababu ya kukosa kucheza mechi nyingi za kucheza kwenye klabu yeka ya Manchester United, na mara ya mwisho kucheza kwenye kikosi cha Southgate, ilikuwa Novemba mwaka jana dhidi ya Scotland.
Kuanza kutemwa kwa Rooney kwenye kikosi, kunaleta shaka juu Nahodha huyo mwenye mabao 53 kwa timu ya Taifa na kuwa mfungaji wa muda wote akiipiku rekodi ya Sir Robert “Bobby” Charlton ya mabao 49 , huenda akashindwa kucheza kwenye michuano ya kombe la Dunia, nchini Urusi mwakani.
“Mara ya mwisho nilisema kuwa amekosa mechi za kucheza, na sasa hivi amecheza kidogo lakini, tumepata wachezaji wanaocheza vizuri, vizuri sana, vizuri kwetu kama Adam Lallana na Dele Alli”. Alisema Southgate.
from Blogger http://ift.tt/2rJidrr
via IFTTT