Kufuati kifo cha mfanyabiashara maarufu nchini Uganda na Afrika Kusini, Ivan Ssemwaga, familia na marafiki wa marehemu wamepinga vikali kuhusu aliyekuwa mkewe, Zarina Hassan kutaka kurithi mali za marehemu.
Hali hiyo imebainishwa na Mtandao wa Big Eye wa Uganda ambao ulimhoji mmoja wa marafiki wa Ivan aliyeeleza hali halisi ilivyo. Chanzo cha habari hii kilisema kuwa Zari amevutana sana na Lawrence Kiyingi ‘King Lawrence’ ambaye alitaka kupora mali za Ivan likiwemo gari la bei mbaya aina ya Lamborghini.
King Lawrence alikuwa rafiki wa karibu wa Ivan na pia ni mwanachama wa kundi la Rich Gang ambalo ni maarufu nchini Uganda kwa kuandaa na ku-host shoo za nguvu.
Chanzo hicho kilieleza kuwa ilifikia wakati madaktari wakawatimua Zari na King Lawrence hospitalini alipokuwa amelazwa Ivan kwa sababu walizua mtiti wakigombana kuhusu mali za Ivan.
“At one point, these fights reached hospital and the two together with other family members had to be thrown out of hospital for the peace and sanity of the sick person. Ivan saw these fights, read some on Facebook but he just could not reply to anything. Someone had to hold the phone for him. And he had no reply just the hissing sounds. Deep down, he must have felt betrayed, used and abandoned by those he considered his closest,” chanzo hicho kilisema.
Zari alionekana kwenye video Instagram akigombana huku akisema kuwa mali za mumewe wa kitambo ni za watoto wake watatu aliowazaa akiwa bado ni mke wa Ivan. Hii ilikuwa siku moja kabla ya Ivan kuaga dunia.
Chanzo hicho pia kilisema kuwa Zari aliwaomba madaktari kuahirisha kutangaza kifo cha Ivan ili aweze kujipanga kabla ili kuwadhibiti wanaopanga kuiba mali za mume wake huyo wa zamani.
Mwanasheria wake aliyetakiwa kuwasiliana naye ili kuweka mipango sawa, alikuwa amesafiri kuelekea Ufaransa ndipo akaomba madaktari wampe siku moja ili kujipanga kabla ya kutangaza msiba huo.
Mrembo huyo alitangaza mwenyewe kifo cha mumewe usiku wa kuamkia juzi Alhamisi baada ya kumaliza kuondoa vitu vyote ndani ya nyumba na kuvihamishia kwingine.
Inasemekana Ivan aliaga dunia Jumanne asubuhi baada ya madaktari kudhibitisha kuwa viungo vyake vya mwili vilishindwa kufanya kazi.
Inasemekana ugomvi wa Zari na familia ya Ivan siyo mpya, ulianza kitambo na chanzo chake ilikuwa ni hizo mali na alichokuwa akiwaeleza ni kwamba mali hizo ni za watoto watatu ambao Zari amezaa na Ivan wakiwa mke na mume.
Kutokana na ugomvi huo, mmoja ya mashabiki kupitia Facebook, alimjibu King Lawrence;
“King Lawrence tafuta maisha yako. Ivan Ssemwanga siyo baba yako. Ivan ana watoto na bado ni wadogo kurithi na kuendeleza mali za baba yao, Zari anaweza kuwasaidia. Ndugu wa Ivan wanaweza kufanya kazi zao wenyewe, acheni kuwa wavivu kugombania mali zisizo za kwenu. Mnataka Zari aachane na mpenzi wake (Diamond) kwa sababu ya mali. Anaweza kuwa na dunia yote……”
from Blogger http://ift.tt/2r3CpDo
via IFTTT