Noma Sana..TCRA Yazikung’uta kampuni za Simu Faini ya Mamilioni ya Pesa..!!!

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya milioni 65 kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya 9,10 na 11 ya kanuni za ubora wa huduma za 2011.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amezitaja kampuni hizo kuwa Benson Informatics Limited Smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar Telecom Limited Zantel, Mic Tanzania Limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania Telecommunications Company Limited, TTCL huku akizitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma bora. 
“TCRA inawakumbusha watoa huduma wote wa mawasiliano nchini kuhakikisha mnatoa huduma zinazokidhi ubora wa sauti na upakuaji wa hali ya juu (Kudownload) pamoja na kufuata sheria za huduma ya mawasiliano ya mwaka 2011”. Alisema Kilaba
Aidha Mhandisi huyo amesema wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma kama ilivyo agizwa.

from Blogger http://ift.tt/2oG8SP8
via IFTTT