Rosa Ree ni rapper wa kike kutoka label ya Navy Kenzo, The Industry.
Akiwa na nyimbo mbili tu hadi sasa, jina lake limeshateka mijadala kwenye vijiwe vya hip hop pamoja na mtandaoni.
Wasanii wakubwa wakiwemo Joh Makini na Diamond wameshanukuliwa wakisema wanamkubali rapper huyo. Video ya wimbo wake mpya, Up In The Air imeendelea kupata airtime ya kutosha kwenye vituo vya runinga vya nje huku wiki hii ukiwa umekamata nafasi ya 5 kwenye chati za muziki wa Afrika ya Soundcity (African Rox Countdown).
Kwa mazingira waliyonayo rappers wa kike Tanzania, hayo ni mambo mambo makubwa ameyafikia hadi sasa.
Hizi ni sababu tatu kwanini Rosa Ree amepata umaarufu:
1. FLOW KALI
Rosa Ree ni bonge la rapper na mwandishi mzuri wa mistari konde. Uandishi wake wenye majigambo mengi na style kali zimemfanya Rosa apate nafasi kwa urahisi.
Kingine ni namna rapper huyu anavyojiamini kupitia mashairi yake na zile attitude halisi za rapper ambaye haoni mwingine zaidi yake – ndio maana anajiita Goddess.
2. VIDEO KALI
Kuna faida kubwa ya kusainishwa kwenye label ambayo inajua kuwa ili msanii wake aweze kufanya vizuri ni lazima uwekezaji mkubwa ufanyike. Video ya wimbo wake uliomtambulisha, One Time iliongozwa na Justin Campos, ambayo isingekuwa rahisi kwa msanii mpya anayejitegemea kuweza kumudu gharama za muongozaji huyo wa Afrika Kusini.
Video yake ya pili, Up in The Air yenye mafanikio zaidi imeongozwa na Hanscana na ambayo muonekano wake unaonesha kuwa gharama kubwa imetumika.
3. AMEJUA KUJIKUSANYIA MASHABIKI WAKE MWENYEWE
Ni ngumu kwa msanii mpya kujikusanyia mashabiki wake mwenyewe katika hatua za mwanzo tu. Rapper huyo taratibu ameanza kukusanya mashabiki wake ambao utambulisho wao unaonekana kwa pozi la kubinua mdomo kama afanyavyo yeye.
Imeandikwa na Fredrick Bundala/Bongo5
from Blogger http://ift.tt/2n6JIKa
via IFTTT