HII Hapa Taarifa Mpya Kuhusu Hali ya Umeme Nchini Kutoka Tanesco..!!

Shirika la umeme Tanzania TANESCO limesema kuwa utunzaji wa vyanzo vya maji vya mto ruaha mkuu ambavyo vinapatikana wilaya za Wanging’ombe na Makete mkoani Njombe unasaidia kuongeza Maji yanayohitajika katika ufuaji wa umeme kwenye mabwawa ya Mtera na Kidatu.
Kaimu mkurugenzio mtendaji wa TANESCO Dr Tito Mwinuka akiwa katika ziara ya kikosi kazi maalumu kilicho undwa Hivi karibuni na makamu wa raisi Samia Suluhu Hassani akiwa mkoani Iringa kwaajili ya kutunza ikolojia ya mto Ruaha mkuu amesema kuwa Asilimia 41 ya umeme unaozalishwa hapa nchini unategemea maji na huwa ni bei nafuu.
Mwenyekiti wa kikosi hicho kilichopangiawa kuzulu vyanzo vya maji vya mto Ruaha mkuu katika mkoa wa Njombe Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe Jackson Ole Saitabau amesema lengo la kikosi hicho kuundwa ni kurudisha hali ya utiririshaji wa maji katika mto ruaha mkuu.
Baadhi ya wananchi wilayani Wangingombe wanaotunza vyanzo mto Ruaha mkuu vya Mbukwa na Mtitafu vilivyoko katika vijiji vya Nyumbanitu, Igima na Mlevela wameeleza changamoto zinazowakabili katika kuhifandhi vyanzo hivyo pamoja na kutoa mapendekezo kwa serikali kusimamia sheria.

from Blogger http://ift.tt/2pODPz1
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2pP8bBB
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2ofJZv0
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2oxackQ
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2pR5BLp
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2pRDAmC
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2oyG6xm
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2oW6Z0N
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2oWGOXT
via IFTTT