Serikali imekiri kuwepo kwa ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hasa katika miji mikubwa nchini ambapo takwimu zinaonesha kuwa Jiji la Dar es salaam linaongoza kwa asilimia 28 ya watoto hao nchini
Hayo yamebainishwa leo Bungeni na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mhe Khatib Said Haji Mbunge wa jimbo la Konde aliyetaka kujua serikali inachukua hatua gani kukabiliana na ongezeko la watoto wa mtaani.
“Ni kweli kumekuwa na ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hasa katika miji mikubwa. Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika katika miji ya Dar es Salaam na Mwanza mwaka 2012 zilionesha kuwa Jiji la Dar es Salaam lilikuwa na watoto 5,600 kutoka mikoa 10 ambayo ni Dar es Salaam 28%, Dodoma 8%, Mwanza 7%, Morogoro 7%, Tanga 6%, Iringa 5% Pwani 5%, Kilimanjaro 5% , Arusha 4%”. Alisema Waziri Ummy
Aidha Waziri huyo amesema serikali ina jukumu la msingi la kuhakisha ulinzi na usalama kwa watoto hao unapatikana pamoja na kushirikisha jamii iweze kuwasaidia kuwaokoa vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi wakiwemo watoto wa mtaani.
from Blogger http://ift.tt/2p9iUt1
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2o9Ntdh
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2p9eWRa
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2o95sBy
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2nI0Zd1
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2nIjMoh
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2nIQxSs
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2o9spEO
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2pylHby
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2pdxaxS
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2pebmlJ
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2nJQi9W
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2ocT6rc
via IFTTT