RAIS wa Benki ya Dunia (WB), Dk Jim Yong Kim anatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa na Jumatatu ijayo akiwa na Rais John Magufuli, wataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu (mzunguko) eneo la Ubungo, Dar es Salaam ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari jijini humo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia, atafanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia keshokutwa na Dk Kim atakutana na Rais Magufuli na kufanya naye mazungumzo muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati baina ya Tanzania na benki hiyo na pia kutembelea miradi ya uwekezaji inayofadhiliwa na benki yake katika miundombinu na kusisitizia haja ya kuendelea kuunga mkono uwekezaji katika maendeleo ya jamii hususani ubora wa elimu na kuwekeza katika elimu ya awali.
Dk Jim akiwa na mwenyeji wake Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa njia ya makutano eneo la Ubungo na pia atatembelea Shule ya Msingi Zanaki iliyopo Upanga.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais huyo wa Benki ya Dunia kutembelea Tanzania.
Benki ya Dunia hivi sasa inafadhili jumla ya miradi 23 ya kitaifa nchini yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.6, na sehemu kubwa ya miradi hiyo inahusika na ujenzi wa miundombinu ya usafiri na miradi ya maendeleo vijijini.
from Blogger http://ift.tt/2mdQOMC
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2mdXASq
via IFTTT