Agness Gerald (Masogange) acheleweshwa na foleni Jangwani, kesi yaendelea

Upelelezi wa kesi ya
kutumia dawa za
kulevya inayomkabili
Msanii Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) katika Mahakama ya Kisutu bado haujakamilika na
imeahirishwa, 
huku akishindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kukwama kwenye foleni. 
Image result for Masogange
Wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliyaeleza hayo leo wakati kesi ilipotajwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, 
Wilbroad Mashauri. 
Mkini alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa hayupo mahakamani hapo.
Baada ya kueleza hayo, wakili wa Masogange, 
Nictogen Itege ameiarifu Mahakama kuwa mteja wako hiyo
alikuwa njiani kuelekea mahakamani lakini alikwama katika foleni eneo la Jangwani.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 20, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa
umekamilika ama la.
Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana  ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA

from Blogger http://ift.tt/2niwRmZ
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2n3VzFu
via IFTTT

Related Posts