Mnajimu na professa wa kilimo Matt Daimon akionekana kukata tamaa baada ya kuachwa kwenye sayari ya Mars: Movie ‘Martian’
Shirika la masuala ya anga pamoja na utafiti na uundaji wa ndege za kisasa kutoka Marekani NASA wanampango wa kupeleka watu kwa mara ya kwanza katika sayari ya Mars ifikapo mwaka 2030. NASA walitoa hivi karibuni taarifa iliyobeba maelezo juu ya mikakati pamoja na mipango ya safari hiyo ya kuelekea katika sayari hiyo ya Mars. Ingawa taarifa hiyo imelalia kwenye upande mzuri wa safari hiyo na wala si nini cha kufanya kama kuna jambo lolote la hatari litawakuta watu ambao watakuwa katika safari hiyo ya kuelekea Mars, inachambua njia chache muhimu ambazo NASA wanatumaini kuziandaa ndani ya miaka 13 iliyobakia. Leo nimekuletea makala hii inayobeba teknolojia 5 ambazo zitatumika kupeleka binadamu wa kwanza katika safari ya Kuelekea Mars #JourneyToMars zifuatazo ni hizo teknolojia 5 ambazo zitatumika:
Roketi kubwa zitatumika
Roketi kubwa na zenge nguvu zinatengenezwa ili kutumika katika safari hiyo
Roketi ambayo itatumika itakuwa ni mbadala wa roketi zinazotumika leo kupeleka wanajimu nje ya dunia. roketi hiyo itakuwa tayari kwa matumizi mwanzoni mwa mwaka 2018 ikiwa na uwezo wa kubeba kilo 70,000 za mahitaji yote ambayo yatakuwa yanahitajika katika safari hiyo. Baadae itatumika roketi nyingine ambayo itabeba mzigo wa kilo 130,000 ambazo zitaitajika pia katika safari hiyo. Roketi hiyo itakuwa na urefu wa futi 382 ni Roketi kubwa kuwahi kutengenezwa pamoja na nguvu zaidi kuliko roketi ya Saturn V ambayo ilitumika kupeleka wanajimu kwenye mwezi.
Mfumo wa injini
Kwa safari hiyo ya Mars ambayo itachukua muda wa takribani miezi 7, kutumia injini za mafuta ambazo zinatumika kwenye roketi za sasa kuleta msukumo unaofanya itembee angani itagharimu fedha nyingi ambazo zitagharimia kwenye uundwaji wa tenki kubwa la kuhifadhi mafuta ya injini hiyo ili kuweza kuirusha ndege hiyo kutoka kwenye ardhi ya dunia.
Badala yake, NASA watatumia nguvu ya jua kama kani ya kusukuma roketi hiyo , wanajimu pamoja na mizigo kwenda ugenini Mars.
Solar Electric Propulsion ndiyo mfumo wa injini utakaotumika kusukuma chombo hicho angani
Njia hiyo inafahamika kama Solar Electric Propulsion itasaidia roketi hizo kubwa kwenda kwa kasi kwa kutoa atoms za ions kwenye injini yake ambayo inawezeshwa na nguvu ya jua. Njia hii siyo ngeni kwani tayari imekwisha tumika kwenye ndege iliyofanya safari ya kwenda kwenye tufe la Ceres lililopo nje ya dunia.
Makazi ya angani pamoja na Mars
Mfano wa picha ya makazi katika sayari ya Mars
Ili wanajimu waweze kwenda Mars na kurudi salama, lazima kuwa na chombo ambacho kitawawezesha wanajimu hao kuweza kuishi ndani ya chombo hicho katika mazingira ambayo yanalingana sawa na yale ya nyumbani(duniani) pamoja na vyoo kwa ajili ya wanajimu waliopakia, pamoja na huko watakapofikia katika hiyo sayari.
Mavazi maalumu ya angani
Wanajimu watakaofika huko watakaa kwa muda wa mwaka mmoja au zaidi kwenye hiyo sayari ya Mars. kwa kipindi hicho, lazima watakuwa wanazunguka katika mazingira ya sayari hiyo, pamoja na kuchukua taarifa za kisayansi kuhusu sayari hiyo ya Mars. Lakini bila kuwa na mavazi maalumu ambayo yaliyodhibitiwa kwa ubora wa juu kuzuia hali ya hewa nyepesi ya sayari hiyo kukutana na binadamu aliyeko huko basi anaweza akafa ndani ya sekunde tu kutokana na hali ya hewa ya Mars ni nzito halafu hakuna Oxygen yakumfanya mtu apumue kama duniani kwa hiyo lazima mtu avae mavazi maalumu ambayo yanamtungi wa oxygen ili kumwezesha kupumua.
Mfano wa suti itakayotumika kuvaliwa na wanajimu katika sayari ya Mars
Suti kama hiyo maalumu imetengenezwa kwa ajili ya kustahimili mazingira ya huko pamoja na miale mikali ya jua, baridi zito na hewa nzito isiyo rafiki kwa binadamu.
Mawasiliano
Muundo wa miale wa mawasiliano utakaotumika kupokea na kutuma taarifa
Sayari ya Mars inapokuwa karibu na dunia umbali unakuwa ni maili milioni 33.9 spidi ya kurusha taarifa za mawasiliano kutoka Mars mpaka duniani ni ndogo, na inahitajika iwe kubwa zaidi, Katika taarifa mpya iliyotolewa na NASA kifaa kidogo kilichopo katika sayari ya Mars kinachofahamika kama Rover ambacho kinafanya utafiti na kuchukua vipimo kwenye udongo wa sayari hiyo kisha kutuma taarifa duniani kinatumia bits milioni 2 kwa sekunde kutuma na kupokea taarifa, Ukilinganisha na kituo cha kimataifa International Space Station cha utafiti na unajimu wa masuala ya anga kilichopo angani spidi yake ya mawasiliano ni bits 300 kwa sekunde, Na ili kuweza kuwasiliana na chombo kilichopo katika sayari ya Mars kwa sasam lazima intaneti yenye nguvu kubwa itahitajika kwa zaidi ya bits bilioni 1 kwa sekunde sawan a Gb 1 kwa sekende. Na hitimisho la suala hilo ni teknolojia ya miale ama ‘lasers.’
Kutengeneza Teknolojia kama hizi kunahitaji fedha nyingi pamoja na muda mrefu wa kufanya utafiti ila wataalamu wanasema shirika hilo la masuala ya anga na uundaji wa ndege kutoka Marekani NASA wanaweza kufanikisha jambo hilo. Japokuwa changamoto nyingi katika safari hiyo ya kuelekea sayari ya Mars 2030.
Nasa wanahitaji watu wakujitolea katika safari hiyo ya kuelekea Mars na mtu yeyote anaweza akaomba nafasi ya kwenda hata wewe lakini awe tayari kwa lolote kwani hii itakuwa kama kujitoa muhanga. Toa maoni yako hapo chini pia usisahau kushare na marafiki ili kusambaza habari hii nao wafahamu.
from Blogger http://ift.tt/2ksb9Ic
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lKMLlV
via IFTTT