Muongoza wa watalii mmoja nchini Tanzania anayetuhumiwa kupotosha tafsiri ya matamshi yaliyotolewa na mtalii leo amefikishwa mahakamani Musoma mkoani Mara baada ya kuwa alikamatwa wiki iliyopita kufuatia agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Simon Sirikwa amefikishwa mahamani leo kwa kile ambacho mamlaka imeeleza kuwa ni kulichafua jina la Tanzania hasa katika sekta ya utalii.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jaffer Mohammed amesema kuwa kanda hiyo ya video ambayo imesambaa kwa wingi katika mitandao ya kijamii imekiuka Sheria ya Makosa ya Mitandao.
Kwa upande wake muongoza watalii huyo alisema kuwa amekuwa akifanyakazi ya kuongoza watalii kwa muda wa miaka 10 sasa na video hiyo walirekodi kama utani tu na hawakuwa na lengo la kuichafua nchi wala sekta ya utalii.
Sirikwa alikamatwa Ijumaa kwenye mpaka kati ya Serengeti na Arusha.
Muongoza watalii huyo alirekodi video nyingine akiwa na mtalii huyo na kusema kuwa walichokuwa wakifanya ni kuchekesha tu na kuwa hufanya hivyo na kuweka kwenye ukurasa wake wa Facebook lakini baadhi ya watu ndio waliichukua video hiyo na kupotosha kupitia mitandao ya kijamii.
from Blogger http://ift.tt/2kOqqXj
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lKO3h8
via IFTTT