JUMLA ya Watanzania 578 wamekamatwa na kufungwa katika magereza ya nchi mbalimbali kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Akiahirisha mkutano wa sita wa Bunge la 11 mjini Dodoma juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alitaja nchi ambazo Watanzania hao wamefungwa kuwa ni pamoja na China (200), Brazil (12), Iran (63), Ethiopia (7) na Afrika ya Kusini (296).
Majaliwa pia alisema vita inayoendelea nchini dhidi ya dawa za kulevya inapaswa kuungwa mkono.
Alisema madawa ya kulevya huingia zaidi kutumia kwa njia za bandari bubu kupitia Bahari ya Hindi na mipakani kwa njia ya magari binafsi na mabasi yatokayo Kenya, Uganda na Zambia.
“Lengo la serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri – wauzaji na wasambazaji,” alisema Majaliwa.
from Blogger http://ift.tt/2kWMrBE
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lDdSQ4
via IFTTT