Na Furaha Eliab, NJOMBE
MAHAKAMA ya mwanzo Kipengele, halmashauri ya Wilaya Wanging’ombe
mkoani Njombe imehamia kwa zaidi ya saa
moja katika kijiji cha Usalule kutazama shamba la mjane Rugina Mwinuka ambalo
miti yake inadaiwa kuibiwa na jirani yake, ambapo imejiridhisha eneo la tukio
na kubaini mabaki ya miti iliyo katwa.
Mjane huyo aliamua kufika mahakamani kufungua kesi baada ya
nmiti iliyo kuwa imepandwa shambani kwake kukatwa na jirani yake Odo Mligo
ambapo kesi iliyo funguliwa ni ya kuvamia shamba na kufanya wizi wa miti
kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu namba 265 sura ya 16 iliyo fanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Hakimu wa mahakama hiyo Mh Mary Kallomo alisema kuwa mahakama
imefika katika eneo hilo kwaajili ya kupata maelezo na kuwa sio kwaajili ya
kupata ushahidi kwa kuwa ushahidi ulisha fungwa mahakamani.
Alisema kuwa kesi hiyo imeirazimu mahakama kuhamia katika
eneo hilo ili kujiridhisha kile ambacho kilielezwa mahakamani na kubaini eneo
hilo kuwa na mabaki ya miti inayo daiwa kukatwa katika shamba la mjane Rugina na
kuhesabu visiki vya miti iliyodaiwa katwa na mkataji.
Mahakama baada ya kuhesabu visiki vya miti vilivyo katwa
katika shamba hili ilibaini kuwa ni mashina 78 wakati Rugina aliiambia mahakama
wakati wa kutoa ushahidi kuwa miti iliyo katwa kuwa ni visiki 55 ambapo
ameiambia mahakama kuwa visiki alivyo vihesabu ni vya upande wa juu huku
vinavyo zidi hakuviona.
Wajumbe wa baraza baada ya kulipima shamba hilo kwa hatua
upana wake walibaini kuwa lina upana wa hatua 111 na urefu ni hatua 140.
Mshitakiwa na mshitaki waliithibitishia mahakama kuwa eneo waliloipeleka
mahakama kuwa ni hili na hawa kupingana na maelezo waliyo yatoa mahakamani.
Hakimu Kallomo aliiahirisha kesi hiyo na kusema kuwa hukumu
yake ni Septemba 31 mwaka huu katika mahakama hiyo ya mwanzo.