WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUKAMILISHA JENGO LA DHAHANATI

KIJIJI cha Ilela kata ya Lupingu wilayali Ludewa mkoa wa Njombe hakina zahanati na hivyo wakazi wake wanategemea huduma kijiji cha Ngrlenge kata ya Manda ambacho nacho kinakabiliwa na na chngamoto ya watumishi na jingo la huduma za mama na mtoto.

Upande wake mganga mkuu wa Zahanati ya Mgelenge Edward Kayuni amesema  imejengwa mwaka 1992 lakini hadi sasa inakabiliwa na changamoto lukuki ikiwa na nyumba moja ya mganga kati ya nane zinazo hitajika.

Amesema Zahanati hiyo inahudumia zaidi ya vijiji viwili ambapo inaukosefu vifaa muhimu mbalimbali vikiwemo na vitendea kazi.

Mbunge wa jiombo la Ludewa Deo Ngalawa anaamua kumpigia simu Mganga mkuu wa wilaya Ludewa ili kujua ujenzi huo utakamilika lini.

Hata hivyo wananchi wanasikitishwa na kutoa michango mingi kwaajili ya ujenzi huo lakini bado jengo hili halija kamilika