POLISI WAOMBWA UDHIBITI WA MADEREVA WASIO NA RESENI

WADAU wa usalama barabarani wameomba jeshi la Polisi kuanza msako wa madereva ambao hawajaenda shule ya masomo ya usalama Barabarani huku madereva wa pikipiki wakitakiwa kutembea na vyeti vya shule walizo somea udereva pamoja na reseni za udereva.



Kauli hiyo imetolewa wa mdau wa usalama barabarani na mkuregenzi wa taasisi ya Apec Respicius Timanywa wakati wa kufunga mafunzo ya udereva Bodaboda ya awamu ya tatu katika mji mdogo wa makambako mkoani Njombe ambapo alisema kuwa madereva wanatakiwa kutembea na vyeti vyao vya udereva ili kutambua walio soma na ambao hawajasoma.



Alisema kuwa madereva wengi wa pikipiki wapo barabarani bado hawajapatiwa elimu ya usalama barabarani na kuwa wengine wakifanya shughuli za udereva kwa kutumia reseni walizo tafutiwa na ndugu zao.



Alisema kuwa jeshi la polisi ili kuwabaini ambao bado hawajasoma inatakuiwa kuwataka madereva wote kutembea na vivuri vya vyeti vyao ili kuhakikisha kuwa wanawabaini wale ambao hawana vyeti na ambao hawajasomea masomo ya udereva.



Timanwa alisema kuwa madereva wa Bajaji ndio wamekuwa wabishi wenda kupata mafunzo ya udereva kwa kuwa kila wanapo toa mafunzo hayo madereva wa Bajaji wamekuwa hawajitokezi huku katika mafunzo waliyo funga Juzi kati ya madereva 297 madereva w abajaji walikuwa chini ya kumi.



Aidha inadaiwa kuwa madereva wa bajaji jarili wao wamekuwa wakiwatafutia reseni za udereva na kusababisha kuwapo kwa madereva wasio na reseni kitu kinacho sababisha madereva wengi kuto jua sheria za usalama Barabarani.



Mgeni rasimi katika hafla hiyo ya kufunga mafunzo katibu tawara msaidizi mkoa wa Njombe Lameck Noah kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe alisema kuwa madereva hao walio na vyeti wakawe waalimu kwa madereva wenzao na kuwataka kuhakikisha kuwa wanawashawishi kwenda shule.



Alitumia fulsa hiyo kuwaasa madereva hao kuwacha mbwembe na mikogo wanapo endesha vyombo vyao kwa kuwa wanaweza kusababisha ajali kwa watu wanao tumia barabara na madhara kwao wao wenyewe kwa kuwa wakiendesha vizuri hakuna atakaye wacheka kuwa hawaendeshi vizuri.



Hata hivyo aliwataka madereva hao kuhakikisha kuwa Kofia ngumu (Helment) ili wateha wao waweze kuzivaa ka kuwa kuna kofia zingiene zimekuwa ni chafu mpaka kutishia abilia wao kupata magonjwa ya ngozi na Mba.



Akisoma lisala kwa niaba ya madereva wengiene Maliamu Mbene alisema kuwa wamekuwa wakiwataka abilia wao kuvaa kosfia ngumu lakini wamekuwa wakikataa kuvaa kofia hizo na kuomba jeshi la polisi kuwakamata abilia wao na sio madereva kawa watakuwa na kofia mbili.