Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Njombe Kusini Jumatatu ya mai 9

MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imesema kuwa baada ya kusikiliza pande zote mbili katika kesi ya kupinga matokeo jimbo la Njombe kusini itatoa hukumu ya kesi hiyo Mai 9 mwaka huu katika ukumbi wa mahakama ya mkoa wa Njombe.

Jaji wa mahakama hiyo Jaji Jacob Mwambegele amesema kuwa kesi hiyo hukumu yake itatolewa Mai 9 na mahakama yake baada ya kusikiliza mashahidi wa pande zote mbili za washitaki na washitakiwa ambapo Juzi kulikuwa na majumuhisho kutoka kwa mawakili kuhusiana na mwenendo mzima wa kesi hiyo.

Wakitoa majumuisho yao mawakili watatu moja kutoka kwa aliye kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Njombe Kusini aliyefungua kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2015 kupinga matokeo yaliyo mtangaza Edward Mwalongo kuwa Mbunge wa jimbo hilo wakili Edwin Swale  huku mawakili wawili wakiwa ni wa upande wa utetezi.

Kwenye majumuisho hayo ambayo yalikuja mahakamani hilo iliyo fanyia vikao vyake katika ukumbi wa mahakama mkoa wa Njombe yalianza kusikilizwa baada ya kufungwa kwa ushahidi ulio tolewa na pande zote ambao walikuwa jumla yao 38 ambako upande wa walalamikaji kulikuwa na mashahidi 16 upande utetezi wa Mbunge wa Njombe Mwalongo kulikuwa na mashahidi 17.

Upande wa serikali ambako walishitakiwa Msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo, Eluminata Mwenda ambaye ni mgurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe na mwana sheria wa serikali ambaye ni msimamizi wa uchaguzi mkoa wa Njombe kulikuwa na mashahidi watano.

Akitoa majumuisho jinsi alivyo isikiliza kesi hiyo na mashahidi wa upande wa mlalamikaji wakili wa Mbunge wa jimbo la Njombe na mshitakiwa wa kwanza, wakili Samson Lutembuka alisema kuwa mashahiti watatu katika kesi hiyo walikuwa ni mashahidi wa kusikia kwa kuambiwa na watu kilichotokea.

Alisema kuwa katika kesi hiyo mlalamikaji na shahidi namba moja alikuwa ni shahidi wa kusikia kwa kuwambia wa watu sio shahidi wa kusikia mwenyewe pia haya hahidi wa pili Zabroni Mwani naye pia hakuwahi kuwashikia wasjhitakiwa wakisema moja kwa moja.

Kwenye kesi hiyo mshitakiwa wa kwanza Mbunge Mwalongo anashitakiwa kwa makosa Mawili ya kutumia kampeni za ubaguzi wa kikabila na kukosea kujaso fomu ya uchaguzi ambapo inadaiwa kuwa mlalamikaji hakuwahi kutoa malalamiko katika kamati ya maadili kitu alicho kisema Lutembuka kuwa kinaipotezea nguvu kesi yake.

Hata hivyo Lutembuka amesema kuwa licha ya kutopeleka malalamiko katika kamati ya maadili mlalamikaji haimzuii kuja mahakamani kulalamika au kupinga matokeo licha ya kuwa ushahidi wake hauta kuwamzito.

Aidha akitoa majumuisho yake Wakili wa serikali   Ntuli Makahesya alisema kuwa wakati akimsikiliza Mlalamikaji alisema kuwa hakusikia hata mahali akisema kuwa alipeleka malalamiko yake kamati ya maadili ya jimbo licha ya chama chake kuwa na mjumbe katika kamati hiyo kitu kinacho mnyimba Mlalamikaji kuwa na nguvua katika kesi yake.

Ntuli alisema kuwa mlalamikaji aliamua kuyaleta haya mahakamani hapa kwa kwua alishindwa uchaguzi, kuto peleka kwenye kamati malalamiko yake madhara ni kuwa na ushahidi hafifu katika kesi yake.

Aidha Ntuli aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali shitaka hilo na kuwa mshitakiwa alipe gharama zote za kuiendesha kesi hiyo.

Akitoa majumuisho yake wakili wa Mlalamikaji Swale amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa batili kutokana na alivyo wasikiliza mashahidi wa upande anao usimamia kwa kuwa vitendo vya ubaguzi ambavyo vingeweza kuchafua hali ya amani ya nchi hivyo mahakana itengue uchaguzi huo kwa ajili ya afya ya nchi.

Alisema kuwa mahakama kama itaona vyema inaweza kuutengua uchaguzi huo endapo itabaini kuwa kulikuwa na vitendo vya Rushwa, ubaguzi, na mgombea  kuto kuwa na sifa vilionekana na kuwa uchaguzi huo hauta kuwa wa kwanza kutenguliwa na mahakama hiyo

Alisema kuwa mahakama kama itaona vyema inaweza kuutengua uchaguzi huo endapo itabaini kuwa kulikuw ana vitendo vya Rushwa, ubaguzi, na mgombea  kuto kuw ana sifa.

Awali Jaji Mwambegele aliwaambia wananchi walio fika mahakamani hapo kuwa kinacho fanywa na mawakili sio kutoa ushahidi bali ni kuuambia umma kile walicho kuibaini katika siku zote za kusikiliza kesi hiyo na kuwataka mawakili kusoma kila kitu walicho mpelekea kama majumuisho yao ili umma kusikia kwa kuwa kesi hiyo ina maslahi kwa umma.


Jaji Mwambegele baada ya kusikiliza pande zote kutoa majumuisho yao alisema kuwa majumuisho hayo sio hukumu na sasa mpira upo kwake na kuongeza kuwa kesi hiyo hukumu yake itatolewa Mai 9 mwaka huu katika Ukumbi wa mahakama ya mkoa wa Njombe ambako mahakama kuu kanda ya Iringa inafanyia vikao vyake majira ya saa 3:00 asubuhi. 

#Elimtaa Tv kuangalia Viteo Bofya Hapa