Zantel yatoa msaada wa kompyuta na huduma ya intaneti bure kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe
0
Kampuni ya simu ya Zantel leo imetoa msaada wa kompyuta 3 na huduma ya intaneti bure kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kwa ajili ya kuwasaidia vijana walio katika kituo hicho kuweza kunufaika na kazi zao kupitia mfumo wa digitali utakaowawezesha kukuza na kusambaza kazi zao.
Kituo cha Mkubwa na Wanawe ni kituo cha kukuza sanaa, kilichoanzishwa mwaka 2011 katika wilaya ya Temeke kwa lengo la kufanya maonyesho ya sanaaa na kutoa fursa kwa vijana wanaoishi kwenye mazingira magumu kuweza kukuza na kuviendeleza vipaji vyao.
Kwa sasa kituo hicho kina idadi ya zaidi ya vijana 102 ambao wana vipaji mbalimbali kama kuigiza,kuimba na kucheza ngoma.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel,Bwana Benoit Janin amekipongeza kituo cha Mkubwa na Wanawe kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuwasaidia vijana wengi kutimiza ndoto zao na hivyo kuweza kuendesha maisha yao.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa akikabidhi msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi akifuatiwa na mwanamuziki kutoka bendi ya Yamoto, Aslay.
‘Sanaa ni ajira kama zilivyo ajira nyingine, na sisi kama Zantel tunaamini msaada huu utawawezesha vijana wengi zaidi kuweza kuboresha na kusambaza zaidi kazi zao za sanaa hivyo kuweza kujikimu kimaisha na kutoa ajira kwa wenzao’ alisema Benoit.
Akielezea zaidi kuhusu msaada huo, Benoit aliwataka wasanii walio katika kituo cha Mkubwa na Wanawe kutumia vizuri vifaa hivyo kuendeleza zaidi vipaji vyao.
Pamoja na msaada huo, Zantel pia itaandaa utaratibu wa mafunzo ya kompyuta na digitali kwa vijana ili kuwawezesha kupata ufanisi na ujuzi katika kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
‘Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na kituo cha Mkubwa na Wanawe katika utekelezaji wa sera ya taifa ya utamaduni inayosisitiza ukuzaji wa sanaa na hivyo kukuza na kuendeleza maslahi ya wasanii’ alisema Mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Bi Leah Kihimbi ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.
Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yusuph Chambuso akitoa shukrani kwa kampuni ya Zantel kwa kuwapa kompyuta na intaneti ya bure. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akifuatiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi.
Naye mwanzilishi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella alitoa shukrani kwa kampuni ya simu ya Zantel kwa kuwatambua uwepo wao na kuwaunga mkono akisema hii ni mara ya kwanza kwa kituo chake kupata msaada kutoka kwa wadau.
‘Kituo chetu kinaona fahari kupokea msaada huu ambao utasaidia vijana wetu na kuwapa fursa ya ya kugundua vipaji vilivyojificha na kuviendeleza kwenye tasnia hii ya sanaa pamoja na kujitangaza zaidi kazi zetu’ alisema Fella.
Tangu kuanzishwa kwake, Mkubwa na Wanawe imefanikiwa kuibua wasanii mbalimbali kama vile Wanaume TMK na bendi ya Yamoto.
‘Kama Mkubwa na Wanawe tumejikita katika kujenga na kuhakikisha vijana wanatimiza ndoto zao na pia kuwasaida wasishawishike au kujishuhulisha na shughuli haramu ambazo zinapotosha maadili kwenye jamii kama vile uvutaji au suuzaji wa madawa ya kulevya na wizi’ alimaliza Fella.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa wa hafla fupi ya makabidiano ya msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kutoka kampuni ya Zantel. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akifuatiwa na Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yusuph Chambuso.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (mwisho kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi wakikabidhi msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kutoka kampuni ya Zantel. Wanaopokea mwisho kulia ni msanii Aslay na Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yusuph Chambuso.
Msanii Aslay akiishukuru kampuni ya Zantel kwa msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo chake cha Mkubwa na Wanawe. Wanaotazama kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi
akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin.
akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin.
Baadhi ya wasanii wa kikundi cha Yamoto Bendi wakionyesha umahiri wao wa kuimba mbele ya wanahabari wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa kompyuta tatu kwa kikundi cha Mkubwa Fella iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.