WANAHISA UTT-PAI WAFANAYA MKUTANO WA WANAHISA DAR

UTT-PID yashiriki mkutano wa mwaka wa Wanahisa wa UTT-AMIS jijini Dar es Salaam

1 (1)
Maafisa masoko wa UTT-PID, Laurence Nzuki (kushoto) na Martin Mchanjila (katikati) wakitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea kwenye banda hilo la UTT-PID wakati wa mkutano huo wa mwaka wa Wanahisa wa UTT-AMIS uliofanyika mwishoni mwa wiki, Novemba 21-22.2015, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Na Andrew Chale, Modewjiblog
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) inafanya miradi mbalimbali ikiwemo huduma za uuzwaji wa viwanja katika maeneo tofauti nchini ikiwemo vile vya mradi wa katika miji ya Chalinze na Mapinga Bagamoyo Mkoani Pwani. Pia mradi wa viwanja vya Bunju, Tundwi songani-Kigamboni ambayo ipo Jijini Dar es Salaam. Mingine ni Kingorwila, Madaganya, Mkoani Morogoro. Lindi, Bukoba, Sengerema na kwingine kwingi hapa nchini.
UTT -PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri na utendaji wa kasi katika utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
AsfOxbUQv7XGaXHM7H-QB4HDmtD0NoXc-5OrHiTpRdSOPicha ya juu na chini Afisa masoko wa UTT-PID, Mary Lugusi akielimisha wananchi juu ya miradi inayoendeshwa na taasisi hiyo kwa wananchi hao waliotembelea banda hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI