MKUU WA KITENGO CHA MIPANGO OFISI YA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI,NKILIJIWANDO ATIMIZA AHADI YAKE KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MISITU JIJINI DAR.



MKUU  wa kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando ambae pia ni mdau wa elimu ametimiza ahadi yake ya kuinunulia Shule ya Sekondari ya Misitu iliyopo kata ya Kivule- Ukonga jijini Dar es Salaam Kompyuta na mashine ya kutolea kopi pamoja na kuchapisha.

Ahadi hiyo ameitimiza leo katika shule hiyo ikiwa aliahidi kipindi walipofanya mahafali ya kidato cha nne katika shule hiyo.

Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu, Pantaleo Maghari amemshukuru  Mkuu wa kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando kwa kuwa na moyo wa kusaidia elimu katika shule hiyo kwani shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na tatizo la kompyuta pamoja na mashine ya  kuchapishia mitihani na kutolea kopi mitihani.

Shule hii inakabiliwa na tatizo la uchache wa meza na viti vya kukalia wanafunzi, mpaka  sasa shule hii ya Sekondari ina wanafunzi 931 ikiwa ina viti na meza 567 tuu. Alisema Maghari

Licha ya hivyo Maghari alisema kuwa pia wanaupungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi, vyumba vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo  ikiwa mpaka sasa wanavymba vya madara 12 tuu na matundu ya vyoo matundu 12 sita sita kwa wasichana na wavulana ambavyo wanafunzi wanatumia kuanzia kidato cha Kwanza mpaka cha nne ambavyo havikidhi mahitaji ya wanafunzi.

Aidha Maghari alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa Elimu kuiangalia shule hiyo ya kata ya Kivyule kwa jicho jingine ili wanafunzi waweze kupata elimu vile inavyotakiwa.
 Mkuu wa kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari ya Misitu iliyopo katika kata ya Kivule-Ukonga jijini Dar es Salaam kulia  ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu, Pantaleo Maghari.
Mkuu wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando akikabidhi baadhi ya msaada wa Kompyuta na (nukushi) Printa katika shule ya Sekondari ya Misitu iliyopo katika kata ya Kivule-Ukonga jijini Dar es Salaam ikiwa ni ahadi aliyoitoka katika mahafari ya shule hiyo. Kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu, Pantaleo Maghari akipokea msaada huo leo shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando akimkabidhi kifaa cha kupunguza umeme Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoiaidi siku ya mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Misitu.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu akipokea baadhi ya vifaa vya Kompyuta kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando leo jijini Dar es Salaam . Nyuma ni wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Misitu wakishuhudia mkuu wao wa shule akipokea msaada huo ili kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakumba walimu kwa kuwa walikuwa nanatumia pesa nyingi kwenda kutoa kopi nyingi za mitihani sehemu nyingine, hivyo basi hawatafanya hivyo kutokana na kutatuliwa changamoto hiyo