Watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (Mwenye shati la batiki) wakiangalia baadhi ya vitabu katika maktaba ya Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakijisajili kwa ajili ya Kozi fupi za Lugha ya Kichina inayotolewa na Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam. Kiktuo hicho kimetoa ofa kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo kujifunza kozi hiyo bila malipo yeyote.Kulia ni Mwalimu wa Kituo hicho Bi. Shen Dongmei.
Watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (Mwenye shati la batiki) wakiangalia baadhi ya picha za kumbukumbu zilizobandikwa katika ukuta wa Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (wa pili kutoka kushoto) akizunguza wakati wa ziara ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China kilichopo Upanga jijini Dar es Salaama jana.Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni Sehemu ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Bw. Liu Dong..
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Lilian Beleko akiuliza swali kwa wahusika wa Kituo cha Utamaduni cha Watu wa China wakati wa ziara ya watumishi wa Wizara hiyo katika kituo hicho kilichopo Upanga jana jijini Dar es Salaam.(Picha na: Frank Shija, WHVUM)