VIJANA TEAM LOWASSA WATANGAZA KUJIONDOA

Habari Star TV Tanzania's photo.
.Baadhi ya vijana waliokuwa wakishiriki kumpigia kampeni Mgombea urais kupitia UKAWA maarufu kama Team Lowassa wametangaza rasmi kutokumuunga mkono kwa madai ya kutotimizwa kwa ahadi walizokubaliana.

Vijana hao wanaundwa na Umoja cha Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Nyegezi jijini Mwanza wakiwemo waendesha pikipiki, mama lishe, Wapagazi, Mawakala wa mabasi yaendayo mikoani pamoja na wajasiriamali wadogo.
Viongozi wa umoja huo wanaamua kukutana hapa lengo likiwa ni kujadili mustakabakali wao katika kumuunga mkono Mgombea huyo.
Ni baada ya aliyekuwa makamu Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi ya Team Lowassa kuwasili mkoani Mwanza na kumuomba kukutana naye ili kujua hatma yao juu ya ahadi zilizotolewa awali.
Baada ya malalamiko hayo, je, nini kauli ya makamu Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa akitumiwa kufanya Kampeni katika mikoa zaidi ya 10?
Hali hiyo inausukuma umoja huo kutoa rai kwa vijana kuwa makini na sera zinazotolewa na wagombea hususani zinazohusu maendeleo yao.
Hata hivyo umoja huo umedai kumuunga mkono Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dokta John Magufuli