Mpekuzi blog
Keshokutwa ni siku itakayokuwa na mambo mengi kwa sababu ya Uchaguzi Mkuu. Pamoja na ratiba ya kila mmoja lakini kupiga kura ni suala linalowaunganisha Watanzania wote. Ili kumchagua rais, wabunge na madiwani, yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:
1.Fika katika kituo cha kupigaji kura katika muda uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambao ni kati ya 1:00 asubuhi hadi 10:00 jioni.
2.Baada ya kupiga kura unatakiwa kuondoka eneo la kupigia kura
3.Usifanye kampeni ya aina yoyote siku hiyo.
4.Usivae sare zinazokutambulisha kuwa wewe ni mfuasi wa chama chochote cha siasa.
Mpekuzi blog