UGUNDUZI WA MAPEMA WA SARATANI YA MATITI UTAOKOA MAISHA YAKO


Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitali za Apollo

Na Mwandishi Wetu,
Saratani inasemwa kuwa chanzo kikubwa cha pili kinachosababisha vifo ulimwenguni. Saratani ya matiti peke yake inaripotiwa kuwa ya pili kama sababu kubwa ya vifo vinavyohusisha saratani kwa wanawake nchini Tanzania. Kuchelewa kupata ugunduzi wa haraka na tiba kwa wagonjwa wengi wa saratani ya matiti kunachangia kuleta ugumu kwenye matibabu pale ugonjwa unapoingia ngazi ya juu zaidi. Gonjwa hili limeendelea kuwa janga hasa kwa nchi zinazoendelea.

Ulimwenguni,mwezi Oktoba ni mwezi maalumu wa kutoa maarifa na elimu juu ya saratani ya matiti. Kwa kawaida tarehe 19 Oktobanikilele cha saratani ya matiti nalengo kuu likiwa ni kutoa maarifa ya msingi na yenye faida kuhusiana na ugonjwa huo. Silaha bora ya kupigana na saratani ya matiti ni kuigundua mapema.
Ongezeko kubwa la namba ya vifo kutokana na saratani linatikisa Tanzania, jinsii navyoathiri namba kubwa ya wanawake kwa sasa. Kutokana na takwimu za hivi karibuni kutoka hospitali ya Ocean Road kitengo cha saratani (ORCI), tafiti zinaonyesha ongezeko kubwa la namba kutoka mwaka 2013-2014 (nusu ya kwanza ya mwaka) zaidi ya kesi mpya  400 zimeripotiwa.