Uchaguzi Umekwisha, Turudi Kwa Wananchi..


Ndugu zangu,
Wakati wowote kuanzia sasa Tume Ya Uchaguzi inatarajiwa kumtangaza John Pombe Magufuli kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano.
Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umefutwa, ni doa, na CCM na CUF Zanzibar hawana namna yeyote
isipokuwa kuitafuta meza ya mazungumzo. Uchaguzi Zanzibar lazima ufanyike, tena haraka.
Tukisubiri hayo, maisha ya kisiasa yanaendelea. Na kazi ya kuijenga nchi kwa kufanya kazi lazima ifanyike.
Kwa vingozi na tunaoshiriki kazi za kijamii tuna lazima pia ya kurudi kwa Wananchi, hususan wa vijijini, kutia shime na kushiriki wenyewe kwenye kuijenga nchi yetu. Kwa kufanya kazi.
Maggid,
Iringa.