NEC Yajibu Malalamiko Ya Ukawa



Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva amejibu malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, kuhusu utofauti kati ya baadhi ya matokeo yanayotangazwa na Tume hiyo na yale yaliyokuwepo vituoni.

Akiongea hivi punde kabla ya kuanza kutangaza matokeo mengine ya majimbo 54, Jaji Lubuva amekanusha taarifa zilizotolewa jana na viongozi wa Ukawa na kutolea ufafanuzi matokeo ya nafasi ya urais yanayopokelewa na kutangazwa na Tume hiyo.

Hivi ndivyo alivyoeleza:

“Tusingependa wakati huu kulumbana na vyama vya siasa au wadau wengine. Hiyo ndiyo nia yetu. Lakini pale panapokuwa na upotoshaji wa hali ya juu, Tume inalazimika kusema machache.
  
"Moja ni upotoshaji unandelea sasa hivi kwamba Tume ya Uchaguzi, matokeo tunayosoma hapa yamechakachuliwa kuhusu wagombea wa urais. 
  
"Hiyo sio kweli hata kidogo, ningependa kutumia nafasi hii kupitia ninyi waandishi wa habari kuelewesha wananchi kwamba wasipotoshwe.

“Nilishawahi kusema kwamba tunachofanya sisi hapa ni kusoma na tumeshahakiki yale ambayo yametokea katika majimbo, hayo ndiyo yaliyokuwa yamehakikiwa wakiwemo mawakala wa vyama mbalimbali. 
  
Updates:
Lowassa  anategemea  kuongea  na  vyombo  vya  habari muda  wowote  mchana  huu.  Endelea  kuwa  nasi
Mpekuzi blog