Mabaa Medi wapatiwa elimu ya mpiga kura Njombe

 Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba akifungua semina ya mpiga kura kwa wahudumu wa baa mkoani njombe

 Washirika wa semina kutika baa mbalimbali za Mjini Njombe

 Mkurugenzi wa Shirika la Njombe Young Development Organization Hamis Kassapa
Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba
Mkuu wa wilaya ya Njombe

WAHUDUMU wa baa (Baamedi) mkoani Njombe wamepatiwa elimu ya uraia na mpigakura ili kufanya zoezi hilo kwa uangalifu na kupata kiongozi bora bila kushinikizwa na mtu yeyote. 

Akifungua semina ya kwa wahudumu hao mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba jana iliyoandaliwa na Taasisi ya Njombe Young Development Organization (Njoyodeo) alisema kuwa wahudumu hao washiriki kwa makini zoezi hilo muhimu kwa mstakabali wa nchi.

Dumba alisema kuwa wanawake wajiamini katika kufanya maamuzi sahihi kwa kusikiliza sera na kufanya maamuzi yao bila kupewa rushwa na kulazimishwa kumchakua mtu fulani wa chama fulani.
 

Alisema kuwa elimu hiyo imefika kwa kuchelewa lakini ni wakati muafaka kwa watu hao ili wafanye uchaguzi kwa usahihi bila kuharibu uchaguzi.

Alisema kuwa uchaguzi huu una muhusi kila mtu na kila kula ya mtu itahesabiwa na inaumuhumu mkubwa kwa kiongozi atakaye chaguliwa kwa m iaka mitano ijayo.

"Kama utapokea rushwa kipindi hiki utapata kiongozi mbovu atakaye kusumbua kwa miaka mitano, hivyo fanyeni uchaguzi sahihi ili kuweza kufanya uchaguzi sahihi," alisema Dumba.

Akitoa elimu kwa wanawake hao wanao fanya kazi katika mazingira magumu ya vishawishi vingi Mgurugenzi wa Taasisi hiyo Hamisi Kassapa alisema kuwa Elimu hiyo wameamua kuitoa ili kuto waingiza katika matatizo kipindi hiki cha uchaguzi.

Alisema kuwa wakipiga kura waende nyumbani na kuendelea na kufanya shughuli zingene kwani wakipata matatizo wakati wa kupiga kura kutokan ana vurugu kiongozi watakaye mchagua hata wakumbuka wala bosi wao wanapo fanyia kazi.

Alisema kuwa wahudumu hao waepuke kuvaa sale ya chama chochote wanapo enda kupiga kura na kuwa wahakikishe kuwa wanapiga kura kwa kiongozi wanayeamini hana mfumo dume huku akiwasihii kuhakikisha kuwa wanafuatilia kampeni na kuzielewa sela za wagombea hasa kwa kutazama na kusikiliza vyombi vya habari.

Naye mmoja wa wahudumu hao Rosemarry Joseph mfanyakazi wa Baa ya Tale, alisema kuwa elimu hiyo hawajawahi kuipata na kuwa wanashukuru kwa elimu hiyo na watakuwa makini kufanya uchaguzi sahihi ikifika siku ya uchaguzi.