Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudentia Kabaka, (kulia), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, wakati wakichukua nafasi
zao kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, jijini Dar es
Salaam, Septemba 4, 2015. Waziri Kabaka alizindua bodi hiyo
itakayoongozwa na Mwenyekiti wake, Bw. Emmanuel Humba.
Waziri Kabaka akitoa hotuba ya uzinduzi wa Bodi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini Bw. Emmanuel Humba akipokea chati cha usajili wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi Kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia
Kabaka (Cheti cha Usajili kimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti
wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini SSRA).
Mwenyekiti wa Bodi, Bw.
Humba, (katikati), akitoa hotuba yake. Kulia ni Waziri Kabaka na kushoto
ni Mkurugeniz Mkuu, WCF, Masha Mshomba
Mgeni rasmi, Waziri Kabaka,
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Mfuko
huo, baada ya uzinduzi rasmi wa bodi.
Waziri wa Kazi na Ajira
Mhe. Gaudentia Kabaka akitoa hotuba kwa Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) pamoja na wageni waalikwa kabla ya kuzindua
Bodi hiyo rasmi.