Mtandao huu umezungumza na kocha mkuu wa kikosi cha ‘wanalambalamba’ Stewart Hall kutaka kujua ni kwanini nyota huyo amekuwa akisugua benchi kwenye kikosi cha Azam tangu ajiunge na mabingwa hao wa Kagame licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu.
“Messi alichelewa kujiunga na timu (Azam) na tayari tulikuwa tumeshaiandaa timu kwa mfumo wetu kulingana na wachezaji tuliokuwanao ambao haukumpa nafasi yeye kwakuwa wakati tunaanza yeye hakuwepo”, amefafanua Hall.
“Baada ya yeye (Messi) kuingia kwenye kikosi cha Azam tukaanza kutafuta namna ya kumuingiza kwenye mfumo mpya na kumpa majukumu mapya. Alipokuwa Simba alikuwa anacheza kama winga lakini kwenye kikosi chetu, mabeki wa pepembeni ndio wanacheza kama mawinga kwahiyo yeye akawa nje ya mfumo”.
“Tulianza kumpa majukumu ya kucheza namba 10 nyuma ya washambuliaji wawili na tangu ameanza kuvaa majukumu hayo amekuwa akifanya vizuri kwenye mazoezi na sasa tumeona ni wakati muafaka wa yeye kucheza kwenye kikosi cha kwanza”.
“Kwa maana hiyo kwenye mchezo wa kesho Messi ataanza kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union baada ya kufanya vizuri kwenye mazoezi”.