RUNGWE CHAUUMA NDIO CHAMA CHA KWENDA IKULU



CHAMA cha Chaumma kimezindua kampeni zake kitaifa huku kikidai kuwa ndicho chama pekee Chenye nguvu kuliko Vyama vya Ukawa chini ya mgombea wake Edward Lowasa na chama cha mapinduzi ( CCM) chini ya Dr John Magufuli
Huku Mgombea Urais akiahidi Ujenzi wa kiwanda cha magari Dar es salaam
Katibu mwenezi wa Taifa wa Chaumma na Mgombea jimbo la Ubungo Bw Kabendera Mbehikya aliyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo zilizofanyika viwanja vya Masenze jijini Dar es Salaam .
Alisema kuwa watanzani wasilewe na mafuriko ya vyama vinavyojiita ni vyama vikubwa alivyoviita vyama vinavyosindikiza Chama chao cha Chaumma Kwenda Ikulu.
" Hivi sasa kuna chama kimoja na nusu ndivyo vyenye nguvu katika uchaguzi huu wa mwaka 2015 chama cha kwanza ni Chaumma na vyama vya CCM na Chadema na washirika wake nusu kwa chama cha Chaumma... Hivyo kuwataka watanzania kuchagua Chaumma na si vinginevyo"
Mgombea mwenza wa chama cha Chaumma Issa Abas Husen alisema kuwa kukosekana kwa viongozi bora ndiko kumelifikisha Taifa katika matatizo haya na kusema dawa ya mafanikio ni kuchagua Hashim Rungwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema kuwa Tanzania ni nchi tajiri ila imeshindwa kupiga hatua kutokana na viongozi wabovu na utawala usio faa wa CCM na kuwa dawa sahihi ni kuchagua chaumma pekee
Hata hivyo alisema chama chake kimejikita zaidi katika sera za kuwakomboa watanzania katika sekta kilimo na Viwanda,afya,elimu pamoja ,kukuza ajira na umoja wa kitaifa
Kwani alisema ni aibu kwa Taifa kukosa kuwa na huduma bora za afya na kushindwa kuboresha sekta ya kilimo.
Huku Mgombea Urais wa Chama hicho Mwanasheria Rungwe akiwaahidi watanzania wanaoonewa kwenda kwake kupata huduma ya sheria ya bure.
Alisema watanzania ambao wamezalisha katika Taifa hili wameendelea kuwa wanyonge katika nchi yao na kuwa baadhi ya nyumba za serikali likiwemo jengo la ubungo Planza yameuzwa kwa pesa ya kutupwa.
Hivyo alisema wakati wa wananchi kupiga kura kwa chama chake umefika na kuwataka kuwanyima kura wagombea wa vyama vingine.
Alisema wapo wengi wanaotaka Ubunge wakiwemo wazee Kama yeye wanaokuja na Sanaa ya kupanda daladala na mabingwa wa kujenga madaraja ambayo si hitaji kwa wananchi.
Hivyo alisema njia pekee ni kuchagua viongozi toka Chaumma pekee chama bora cha ukombozi.
Alisema yeye ni mtanzania wa kwanza kuleta kuuza magari Tanzania na wakimchagua magari tatatengenezwa Tanzania ili kukuza ajira
Alisema kuwa lazima serikali ya Chaumma kuhakikisha kiwanda cha magari kinajengwa jijini Dar es Salaam ili kukuza ajira zaidi na kuondoa usumbufu wa kuingiziwa magari mabovu