MGOMBEA Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia anaungwa mkono
na vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na NLD, Edward Lowassa amesema endapo atachaguliwa kuwa rais
ataunda serikali isiyokuwa ‘nyoronyoro’.
Akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Kawe jijini Dar
es Salaam katika viwanja vya Shule ya Msingi
Bunju ‘A’, Lowassa alisema muda umefika kwa
wananchi wa Tanzania kufanya mabadiliko.
“Naombeni mniteue niwe rais wenu ili mpate
maendeleo ambayo hamkuwahi kuyapata kwa
kipindi cha miaka zaidi ya hamsini. “Mimi nitaunda
serikali isiyokuwa nyoronyoro na inayofanya kazi
zake kwa ufanisi na kila mtanzania ataweza
kunufaika na rasilimali za nchi yake,” alisema
Lowassa aliyehutubia kwa takribani dakika kumi.
Alisema endapo atafanikiwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano, serikali yake itafanya kazi kwa spidi ya
mwendo kasi wa 120 na hivyo lazima kutakuwa na maendeleo makubwa kwa muda mfupi.
9/8/2015 Lowassa aahidi utendaji spidi 120 | 2jiachie - Official Site
http://www.2jiachie.com/2015/09/lowassa-aahidi-utendaji-spidi-120.html 2/8
Share ! Tweet 0 Like 0 1
“Nitaondoa changamoto zote zinazowakabili wananchi wa Tanzania, ikiwemo ukosefu wa huduma ya maji
safi na salama katika maeneo mengi hapa nchini, nitatatua changamoto ya mazingira ya kufanyia
biashara ndogondogo pamoja na kutoa elimu bure,” alisema Lowassa.
Aidha, aliwahakikishia wananchi kuwa wasiwe na hofu kuwa kura zao zitaibwa, akisema, “Hakuna
atakayeiba kura ng’o. Nimesikia kuwa kuna njama za kuiba kura, hakuna jambo kama hilo, bali kila mtu
akipiga kura ahakikishe analinda kura hadi mwisho ili kutoruhusu mwanya wa kuiba na hakuna
atakayeiba kura ng’o.”
Awali, akimkaribisha Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alisema wamezunguka
katika baadhi ya maeneo ya nchi na kuona watanzania wamechoka na ugumu wa maisha na hivi sasa
wanataka mabadiliko.
“Watanzania wanahitaji mabadiliko, tumepata mapokezi makubwa sana kila tulipopita kuomba ridhaa ya
wananchi, hii inaonesha ni jinsi gani wananchi hawa wapo tayari kukombolewa,” alisema Mbowe.
Mbowe aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na kuchagua Chadema ili
kiwakomboe na kutatua changamoto zinazolikabili taifa. Baada ya kutoka Kawe katika Manispaa ya
Kinondoni, jioni Lowassa alikwenda katika jimbo lingine la manispaa hiyo, Kibamba, kuendelea na
mkutano wa kampeni.
CHANZO: HABARI LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)