Askali wa usalama barabarani wafunguliwe miradi kuepuka rushwa

MKUU wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi amemshauri kamanda wa polisi mkoa huo Wilbroad Mtafungwa kuanzishwa miradi kwaajili ya Jeshi la polisi ili kuepusha vitendo vya rushwa hasa kwa askali wa barabarani.

Ushauri huo umetolewa wakati wa siku  ya kilele cha wiki ya usalama barabarani Mkoani Njombe ambapo kamanda wa polisi mkoa huo alisema kuwa Polisi wake wamekuwa wakilalamikiwa kwa vitendo vya rushwa.

Dr. Nchimbi alisema kuwa wamekuwa wakilalamikiwa polisi kwa kuwa hakuna miradi ambayo inawaingizia kipato huenda maralamiko hayo yakiwa na ukweli ama sio ya ukerli.

Alisema kuwa jeshi la polisi linatakiwa kufungua miradi kwaajili ya askali wake il;I kutokuwa na tama ya kupokea pesa kutoka kwa madereva kama wanavyo lalamikiwa.

Alisema kuwa kwa sababu mkoa wa Njombe una ardhi nzuri kwa kilimo polisi wanatakiwa kuwa na mashamba ya miti au ufugaji wa nyuki kwaajili ya kujiingizia kipato chao cha kila siku na kuachana na vitendo vya rushwa na kuondokana na malalamiko ya vitendo vya rushwa.

Aidha awali akimkaribisha mkuu wa mkoa, kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Mtafungwa alisema kuwa mitaani kumekuwa na malalamiko ya upokeaji wa rushwa kwa askali wa jeshi polisi wa usalama barabarani.

Alisema malalamiko hayo huenda yana ukweli ndani yake ama hayana ukweli kwa kuwa hakuna mwenye udhibitisho juu ya upokeaji na utoaji wa rushwa kwa askali hao.

Kwa upande wao baadhi ya madereva Mkoani humo wamesema kuwa wamekuwa wakikutana na vitendo hivyo huku wakiambiwa wajiongeze.

Akizungunza baada ya kufungwa kwa siku ya usalama barabarani Hezron Raison dereva wa daladala Mkoani Njombe alisema kuwa wakekuwa wakinyanyashwa na baadhi ya askali wa barabarani kwa kutozwa pesa bila ya kuwa na kosa lolote na kuwambiwa wajiongeze.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya madereva wamekuwa wakiendekeza rushwa rushwa baada ya kuona wamefanya kosa wanatoa pesa ili waachiwe.