Wagombea CCM wajipanga kupambana na wagombea wa Upanzania


WAGOMBEA ubunge waliopita katika kura za maoni wilaya ya Njombe yenye majimbo matatu, kupitia chama cha mapinduzi CCM wamesema kuwa baada ya kufunguliwa kwa mampeni mpaka uchaguzi wataingia kusinda na sio kushindana.

Wakizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo wagombea hao walisema kuwa vyama vya upinzani vitakuwa na mbio fupi kwa kuwa wanaimani na kazi zilizofanywa na chama hicho na wananchi wanaimani nao.

Edward Mwalongo mgombea wa ubunge aliyepita katika kura za maoni katika jimbo la Njombe kusini lililokuwa chini ya Spika wa bunge Anna Makinda alisema kuwa jina likirudi kupelerusha bendera ya chama hicho wapinzani mbio zao zitakuwa fupi kwa kuwa hakuna walichoi kifanya na chama chake kuana mambio ya maendeleo kimefanya.

Alisema kuwa uchaguzi huu utakuwa rahisi kwa kuwa mambo yaliyo fanywa yanaonekana wazi na kuwa watashinda kwa kishindo na kuwa chama hicho kina watu wengi tofauti na wanavyo fikili wapinzani.

Aidha aliwaomba wanaCCM kuweka mshikamano wakati wa kampeni na uchaguzi na kuunganisha nguvu kutoka kwa wagombea wote walioshiriki katika kura za maoni ili kutoliachia jimbo hilo kwenda kwa wapinzani.

Kwa upande wake mbunge anaye tetea kiti chake wa jimbo la Makambako Deo Sanga alisema kuwa anawashukuru wana CCM walio mpigia kura katika jimbo lake na kuwa anawaahidi wanachama hao na wanaMakambako wote akiingia tena bungeni atahakikisha kuwa anakamilisha mipango aliyo kuwa ameianza akiwa mbunge.

Alisema kuwa wapinzani wajiandae kushindwa na sio kushinda kwa kuwa katika jimbo hilo maendeleo yanaonekana wazi wazi.

Naye mgombea wa jimbo jipya la Lupembe, Joram Hongoli alisema kuwa anashurukuru kwa imani waliyo mpa wananchi wa jimbo hilo jipya kwa kumteuwa katika kura za maoni na kuwa anawaahidi kutekeleza ilani ya chama hicho na kuwa wapinzani wajipange kwelikweli kwa kuwa atatemba katika maendeleo yaliyo fanywa na mtangulizi wake Sanga ambaye kwa sasa yupo katika jimbo la Makambako ambalo awali lilikuwa moja mpaka jimbo lake na liliitwa njombo la Njombe Kaskazini.