Usafi wa mazingira


HALMASHAURI ya mji Njombe imewaweka wadhabuni wawili katika seka ya usafi ili kuhakikisha usafi unaimarika katika mji huo ambao kuwa sheria ya utupaji taka imeanza kutekelezwa na faini kwa wanao tupa taka hovyo.

Akizungumza na Nipashe Mkoani Njombe afisa mazingira mji wa Njombe Dolnald Mwalongo alitoa ufafanuzi huo baada ya wananchi wa mji huo kuibua malalamiko ya kuchangishwa fedha na mdhabuni bila ya wao kujua na kuhofia kutapeliwa.

Mwalongo alisema kuwa halmashauri hiyo imeanzakukusanya fedha kuwa kutumia mdhabuni na kuzizoa taka hizo kwa kutumia mdhabuni wa kampuni mbili tofauti.

Alisema kuwa kwa kawaida mwananchi au mdau wa uzalishaji wa taka anatakiwa kuchangia kwa asilimia fulani ili kuzitoa kutoka vizimba vya taka na kuzipeleka mbali na mji.

Alisema kuwa halmashauri pesa imeamua kuweka wadhabuni wawili katika seka hiyo ya usafi wa mazingila ili kuboresha usafi wa mazingira.

Alisema kuwa imeweka wadhabuni wawili ili kutekeleza majukumu ya usafi ya mazingira katika mji huo huku Akieleza kuwa mdhabuni wa kukusanya pesa anapita kila sehemu anayo takiwa kupita na kukusanya pesa na mdhabuni wa pili ni kutoa kata katika vizimba vya taka na kuzipeleka katika dampo kuu la mji huo.

Aidha kwa upande wao wananchi walisema kuwa hawajatambulishwa na Mkurugenzi kupitia watendaji wao wa mtaa juu ya mzabuni anaye kusanya pesa.

Baadhi ya wananchi wamedai kuwa wanakwepa kulipa malipo ya utoaji taka kutokana na mdhabuni hiyo kuto fahamika na kuhofia kutapeliwa.

Felix Mwabile ni mmoja wa wafanyabiuashara kwa ufahamu wake anasema kuwa kazi ya kukurugenzi ni pamoja na kutoa taka katika vizimba na kuwa kazi za wananchi ni kuzipeleka katika maeneo ya vizimba vya taka.

Hata hivyo licha ya wananchi kutokuwa na taarifa za mdhabuni huyo mwenyekiti wa mtaa wa National Housing mjini Njombe Malaki Chaula alisema kuwa ofisi yake imepokea barua ya uwepo wa mdhabuni atakaye kuwa anahusika na ukusanyaji wa taka kutoka kwa Mkurugenzi.