TANZANIA TUOMBE TUSIFIKE HUKU !!! SABABU TANO ZINAZOZUIA UPATIKANAJI WA AMANI YA KUDUMU SUDAN KUSINI NDIYO HII.


Mkutano wa IGAD PUSL 

Kwa upande wao Upinzani nao unataka kuwa na usemi mkubwa zaidi katika serikali mahuluti

Mashirika ya kupigania haki za kibinadamu nazo zimepinga mkataba huo wakisema kuwa unatilia sisitizo kwa ugavi wa mamlaka miongoni mwa mabwenyenye wachache wala sio kusisitizia kuwepo kwa njia ama mbinu za kuwawajibisha viongozi wakuu katika serikali hiyo na yeyote ile itakayokuwa uongozini Juba.

Aidha wangependa chimbuko la mzozo huu ushughulikiwe ilikuzuia mapigano siku za usoni mbali na kuwachukulia hatua wale wote ambao wametenda makosa ya kivita Sudan Kusini.

Kibwagizo ni kuwa mpango huo wa kusitisha mapigano haupaswi kuangaliwa ni kama ndio suluhisho la vita ila utumiwe kama mwanzo wa makubaliano ya amani baina ya pande zote hasimu.

3. Mataifa jirani ya Sudan Kusini Viongozi wa mataifa jirani na Sudan Kusini wamekuwa wakijaribu kuleta amani baina ya mahasimu hao wawili lakini bila mafanikio. 

Katika kipindi cha mwaka mmoja u nusu uliopita viongozi wa mataifa jirani na Sudan Kusini wamekuwa wakijaribu kuleta uwiano baina ya mahasimu hao wawili lakini bila mafanikio.

Hii imetokana na kuwepo kwa ushawishi fulani na uhusika wao kwa njia moja au nyengine na hali ilivyo huko Sudan Kusini.

Uganda kwa mfano ilituma majeshi yake kuilinda mji mkuu wa Juba.

Sudan kwa upande wake imewaruhusu wapiganaji waasi kukita kambi zao ndani ya mipaka yake mbali na kuwahami kwa silaha nzito nzito.

Kenya kwa upande wake ingependa kujishirikisha kwa sababu za kiuchumi huku Ethiopia ikisisitiza kuwa ingependa kuongoza mpango wowote wa amani.

4. Kusambaratika kwa waasiUasi chini ya bwana Machar ulikuwa wa kipekee;makundi ya waasi ambao walikuwa wamekosana na serikali kwa sababu moja au nyengine yaliungana na kuishambulia serikali.

Kulikuwa na makundi ya raia waliojihami kwa silaha na vilevile kulikuwa na baadhi yao ambao walikuwa ni wanajeshi walioasi jeshi la taifa la SPLA.

Kwa hivyo alipotangaza kujitenga na kundi linaloshirikiana na Machar, Jenerali Peter Gadetand Gathoth Gatkuoth alidai kutengwa na Machar. Jenerali Peter Gadetand Gathoth Gatkuoth alidai kutengwa na Machar. 

Gatkuoth alidai hakufurahia kuwa Machar alikuwa anafanya mazungumzo ya kurejea serikalini na kugawana mamlaka na hasimu wao mkuu rais Salva Kiir.

Je iwapo makundi ya waasi yamegawanyika wale wanaomuunga mkono jenerali muasi Gatkuoth alidai ni wangapi ? na wanauwezo wa kutibua makubaliano ya amani ?

Hilo ndilo linasubiriwa kubainika huko Ethiopia.Mamilioni ya raia wa Sudan kusini wamezaliwa katika vita. 


Vita vya kwanza kati ya waasi wa Kusini na Serikali ya Kaskazini vilidumu kwa muda mrefu kati ya mwaka wa 1955-1971.

Kizazi kizima cha raia wa Sudan Kusini walizaliwa na wakabalehe vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiendelea.

Mara ya pili vita hivyo vilipoanza vilidumu kwa kipindi kirefu zaidi yaani kati ya mwaka wa (1983-2005).

Kwa hivyo vizazi viwili vya wananchi wamezaliwa katika vita , kiasi cha kuwa hata baada ya kupata uhuru wake mwaka wa 2011 amani haikudumu kwa zaidi ya miaka miwili.

Vita vinavyoendelea hadi sasa vilianza desemba mwaka wa 2013.

Ubabe kati ya watu wa kabila la wa- Nuer na wa- Dinka, ndio uliotawala siasa za taifa hilo.

Inaaminika kuwa watu wa kabila dogo la Bul Nuer waliisaidia serikali kukabiliana na jamii kubwa ya wa-Nuer hii ni kumaanisha kuwa sasa kuna uhasama baina yao na jamii ya watu wa kabila la Nuer.

Na kwa sababu matabaka mawili makubwa yamekuwa yakipigana na kulipiziana kisasi inakuwa shida mno kupata amani ya kudumu.BBC