Taarifa ya kuwapo kwa Mvua kubwa


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu ya mdomo: +255 22 2460735/2460706
Nukushi: +255 22 2460735/2460700
Baruapepe: met@meteo.go.tz
Tovuti: www.meteo.go.tz S. L. P 3056,
DAR ES SALAAM.
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 28 Agosti, 2015
TAARIFA KWA UMMA:
TAARIFA ZISIZO ZA KWELI ZA UWEPO WA MVUA KUBWA NA
UPEPO MKALI KATIKA MAENEO YA DAR ES SALAAM, PWANI,
TANGA, UNGUJA NA MTWARA
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inawatahadharisha wananchi kuhusu
taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya Kijamii inayohusu uwepo wa upepo
mkali utakao vuma kwa kasi ya km 123.7 kwa saa na mvua kubwa kwa siku ya
tarehe 29/08/2015 kuanzia saa 7 mchana. Taarifa hii si ya kweli na kuwa
Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) haijatoa TAHADHARI hiyo.
Utabiri sahihi wa kesho tarehe 29/08/2015 katika maeneo hayo ni kama
ifuatavyo: Mvua nyepesi zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo hayo( Dar es
Salaam, Pwani,Morogoro, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba).
Upepo unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya wastani wa kilometa 30 kwa saa katika
pwani ya kaskazini( Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja
na Pemba) na kwa kasi ya kilometa 20 kwa saa katika pwani ya kusini(Mtwara).
Aidha, Mamlaka inapenda kuujulisha umma kuwa ina utaratibu maalumu wa
kutoa tahadhari kwa kutumia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii
https://www.facebook.com/tmaservices,https://twitter.com/tma_services,
https://www.youtube.com/user/TanzaniaMetAgency,
http://tma.meteo.go.tz/cap/en/alerts/rss.xml, http://meteotz1950.blogspot.com/ na
tovuti yetu http://www.meteo.go.tz/ hivyo basi Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania inatoa wito kwa umma kuacha kutoa na kusambaza taarifa za
kupotosha katika mitandao ya kijamii.
Imetolewa na:
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA