TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


   “PRESS RELEASE” TAREHE 28.08.2015.



·        MTU MMOJA ANAYEDHANIWA KUWA NI MHALIFU AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI.

·        MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA B AADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.

·        JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUCHANA BENDERA YA CHAMA NA KUBANDUA BANGO LA MGOMBEA.


·        JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA DAWA YA KULEVYA [BHANGI].





KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ANAYEDHANIWA KUWA NI MHALIFU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA ATHUMANI ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA DORIA ENEO MLIMA NYOKA NJE KIDOGO NA JIJI LA MBEYA NA KUFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO ENEO LA MLIMA NYOKA, KATA YA ITEWE, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
UCHUGUZI UNAFANYIKA KUPATA UKWELI WA SABABU ZILIZOPELEKEA MAUAJI HAYO, KWANI ZIPO TAARIFA ZINAZODAI KUWA MAREHEMU NA WENZAKE WATATU NI BODABODA NA WALIKUWA WAKISINDIKIZA LORI LILILOKUWA LIMEBEBA SHABA BILA KUWASILIANA NA ASKARI WALIOKUWA DORIA ENEO HILO AMBALO UWA  NA MATUKIO YA UHALIFU YA MARA KWA MARA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. ASKARI POLISI WALIOKUWA KWENYE ENEO LA TUKIO PAMOJA NA WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO WANAHOJIWA KUPATA UKWELI. UPELELEZI UNAENDELEA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMBINISYE MWANDOBO (65) MKAZI WA KISEGESE ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISSION ITETE KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KISEGESE, KATA YA KISEGESE, TARAFA YA PAKATI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA AJALI. UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/KANUNI/ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.






KATIKA TUKIO LA TATU:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMANI JOHN @ MWAKASEGE KWA KOSA LA KUHARIBU MALI [KUCHANA PICHA] YA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO ILOMBA, KATA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MTUHUMIWA ALIONEKANA AKIWA AMEBEBA MABANGO YA PICHA ZA MGOMBEA WA URAIS HUKU YAKIWA YAMECHANWA VIPANDE VIPANDE NA NDIPO JITIHADA ZA KUMKAMATA ZILIFANYIKA NA KUMFIKISHA KATIKA KITUO KIDOGO CHA POLISI ILOMBA.
AIDHA KATIKA TUKIO JINGINE, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FADI MWASHIMAHA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUHARIBU MALI [KUCHANA BENDERA YA CHAMA CHA MAPINDUZI].
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.08.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO IYUNGA, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MTUHUMIWA NA VIJANA WENGINE WALIITOA BENDERA HIYO ILIYOKUWA JUU YA MTI NA KISHA KUICHANA KWA MADAI KUWA MTI HUO ULIOKUWA UMEFUNGWA BENDERA HIYO NI MALI YAO.
WATUHUMIWA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO HII KUTOKANA NA MAKOSA HAYO.

TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NSAJIGWA BROWN (23) MKAZI WA ITUNGE 2. AHOBOKILE RUBEN (21) MKAZI WA ITUNGE NA 3. AYUBU CHURA (25) MKAZI WA BONDENI – WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 25.
WATUHUMIWA YA WALIKAMATWA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:30 HUKO ENEO LA BONDENI, KATA YA KYELA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.