WAANDISHI wa habari
hapa nchini wametakiwa kuwa makiti katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa kufanya
kazi zao kwa taharadhari kwani wanakazi wakati wa uchaguzi na wataendelea kuwa
na kazi baada wa uchaguzi.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa
habari Mkoani hapa, Njombe Press Club, Mecy Sekabogo, katika mkutamo mkuu wa
waandishi wa habari Mkoani humo.
Alisema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakifanyakazi bira
tahadhari na kupata na madhara ya majeraha, kuharibiwa vifaa vyao na wengine
kuuwawa kusha vyombo vyao kuwakana.
Alisema kuwa waandishi katika kipindi hiki wanatakiwa
wasijiweke katika siasa bali wafanye kazi za siasa kwa kuto pendelea upande
wowote wala kuvaa nguo za baadhi ya vyama.
Alisema kuwa waandishi wapo kila siku lakini kipindi cha
uchaguzi kina pita na kuwa waandishi wataendelea kufanya kazi hata baada ya
uchaguzi kupita.
Sekabogo (Pichani Mwanamama) alisema kuwa uandishi wa mtu utaendelea hata baada ya
uchaguzi kwani wanasiasa wamekuwa wakiwatumia watu kwa kujinufaisha wenyewe na
baada ya kushindwa huwaacha waandishi na kuangalia mamboyao.
Alisema kuwa hatarajii kuona makaburi baada ya uchaguzi mkuu
anatarajia kuendeleza kuona waandishi wapo na kuendeleza na kazi yao ya
kuandika habari za kijamii.
“Katika kipindi hiki waandishi hamtakiwi kuwa upande wowote
kwa kuwa utwtwkiwa kwenda kuandika habari za chama kingigine hauta andika
vizuri kwa kuwa upo katika chama kingine,” alisema Sekabogo
Aidha kwa baadhi ya waandishi wamesema kuwa wamefurahia
kukumbushwa juu ya tahadhari wanazo takiwa kuzichukua wakati wa kipindi hiki
cha uchaguzi na kuwa watakuwa makini na kuto kuwa makaburi baada ya uchaguzi
mkuu.