Kenya yashindwa kwenye Marathon




Ghirmay Ghebreslassie, ndiye aliyeizolea Eritrea medali ya kwanza ya dhahabu
Wanariadha wakenya waliambulia patupu katika mashindano ya mbio za marthon za kufungua makala ya mwaka huu ya mashindano ya riadha ya dunia huko Beijing China.
Tineja kutoka Eritrea , Ghirmay Ghebreslassie, ndiye aliyeizolea Eritrea dhahabu ya kwanza ya makala ya 15 ya mashindano haya aliposajili muda bora wa saa mbili na dakika kumi na mbili(2:12:27).
Ghebreslassie alitoka nyuma na kumpiku mwanariadha kutoka, Lesotho Tsepo Ramonene, katika hatua ya kilomita 42 .
Wakati huo Yemane Tsegay, wa ethiopia ndiye aliyekuwa ameshindwa na kasi na joto iliyokuwa imewazidi wanariadha wengi watajika.
Tsegay hatimaye aliridhika kwa nishani ya fedha alipomaliza mbio hizo akiandikisha muda wa saa mbili 2:13:07
Mwanariadha kutoka Uganda Solomon Mutai (2:13:29)ndiye aliyetamatisha orodha ya tatu bora na kuwanyamazisha wakenya ambao walikuwa wamepigiwa upatu kusajili muda bora na kutawala mbio hizo za kwanza katika uwanja wa Birds Nest ulioko Beijing.
Amini usiamini,mwanariadha wa kwanza raia wa Kenya alimaliza mbio hizo katika nafasi ya 22 naye alikuwa ni bingwa wa mbio za Paris Marathon Mark Mutai.
Amini usiamini,mwanariadha wa kwanza raia wa Kenya alimaliza mbio hizo katika nafasi ya 22
Aliandikisha muda wa saa mbili na dakika 21. 2:21:19 .
Kabla ya kuanza kwa mashindano hayo Kenya ilikuwa imewasilisha kikosi kilichojumuisha mshikilizi wa rekodi ya dunia
Dennis Kimetto (2:02:57), Bingwa wa mbio za Marathon za Chicago na vilevile Berlin, Wilson Kipsang (2:03:23) na vilevile mshindi wa mbio za marathon za
London na New York.